Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Unavyoathiriwa na Tekinolojia ya Kutunza Siri!
    Amkeni!—2009 | Agosti
    • Leo habari nyingi zinahifadhiwa kupitia kompyuta, kuweka pesa katika benki, kutuma pesa, malipo mbalimbali, pia rekodi kuhusu tiba, biashara, na serikali zinalindwa kupitia maandishi ya siri. Habari hizo za siri zinasomwa na wale ambao wana ufunguo wa kuzirudisha katika hali ya kawaida.

      Ufunguo wa chuma una mabonde mbalimbali, ufunguo wa kompyuta ni mchanganyiko wa nambari sufuri na moja zilizofuatana. Ufunguo mrefu una mchanganyiko wa nambari nyingi zaidi, na inakuwa vigumu kuutangua. Kwa mfano, ufunguo wenye nambari nane, unaweza kuchanganywa mara 256, lakini ufunguo wenye nambari 56 unaweza kuchanganywa zaidi ya mara quadrillion 72. Kwa sasa ufunguo wenye nambari 128 ndio unaotumiwa kuficha habari kwenye Intaneti. Ufunguo huo unaweza kuchanganywa mara sextillion 4.7 zaidi ya ufunguo wenye nambari 56!a

      Hata hivyo, bado maneno ya siri hutanguliwa. Kwa mfano, mnamo 2008, waendesha-mashtaka wa serikali nchini Marekani waliwashtaki wanaume 11 kwa kile kinachosemekana kuwa wizi mbaya zaidi wa vitambulisho. Ilisemekana kwamba wezi hao walitumia kompyuta, tekinolojia isiyotumia nyaya, na programu fulani za pekee za kompyuta ili wapate namba za kadi za benki watu walipokuwa wakizitumia kulipa.

      Je, Habari Zako za Siri Ziko Salama?

      Ni kweli kwamba si rahisi kutangua maandishi ya siri yanayolinda akaunti yako ya benki na ununuzi unaofanya kupitia kompyuta. Lakini mengi yanakutegemea. Biblia inasema: “Mtu mwerevu ni yule ambaye ameona msiba na kujificha, lakini wasio na uzoefu wameendelea mbele nao lazima waumie.” (Methali 22:3) Kwa hiyo, uwe mwerevu na “kujificha” ili usiibiwe au kufanyiwa ulaghai kwa kuchukua hatua zifuatazo:

      ◼ Tumia programu za kompyuta za kuzuia virusi.

      ◼ Weka programu za kutambua mtu anapotaka kuingia katika kompyuta yako.

      ◼ Weka programu ya kumzuia mtu asiingie katika kompyuta yako.

      ◼ Hakikisha kwamba programu zilizotajwa juu ni za kisasa kila wakati, na uweke mfumo kuboresha ulinzi kila wakati.

      ◼ Jihadhari na mialiko ya kutumia Intaneti inayotumwa kupitia barua-pepe au ujumbe mfupi, hasa ikiwa barua hiyo inatoka kwa mtu usiyemfahamu na inaomba utume habari za kibinafsi au utume neno au namba ya siri ya utambulisho.

      ◼ Unapotuma habari muhimu sana, kama vile habari kuhusu kadi ya benki, tumia vituo vya Intaneti vyenye uwezo kuficha habari, na ufunge kituo hicho mara tu unapomaliza.b

      ◼ Chagua neno au namba ya siri ya utambulisho ambazo si rahisi mtu afikirie, na uzilinde.

      ◼ Usinakili au kutumia programu za kompyuta kutoka katika vyanzo usivyovijua.

      ◼ Uwe na kawaida ya kunakili habari zako, na uzihifadhi mahali salama.

      Ukifuata hatua hizo za msingi za kujilinda na nyingine zozote zinazofaa sasa au wakati ujao, utakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kulinda habari zako za siri.

  • Unavyoathiriwa na Tekinolojia ya Kutunza Siri!
    Amkeni!—2009 | Agosti
    • a Quadrillion ni nambari 1 ikifuatwa na sufuri 15. Sextillion ni nambari 1 ikifuatwa na sufuri 21.

      b Vituo vya Intaneti vyenye uwezo wa kuficha habari vina ishara fulani, kama vile ishara ya kufuli au “https://” kwenye kisanduku cha anwani. Herufi s inamaanisha salama (secure).

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki