Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maoni Yanayofaa Kuhusu Faragha
    Amkeni!—2003 | Januari 22
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 11]

      Jihadhari!

      HABARI ZA SIRI NA VITUO VYA INTERNET VYA WANAOTAFUTA KAZI: Watu wanaotafuta kazi kwa kuweka maelezo ya elimu na uzoefu wao wa kazi kwenye Internet hukabili hatari ya habari zao kusambaa kwa wengine. Habari hizo zinaweza kuhifadhiwa kwa miaka mingi kwenye Internet na zinaweza hata kutumiwa na wezi wa vitambulisho. Vituo fulani vya kutangaza kazi huomba habari za kibinafsi za watu wanaotafuta kazi kama vile, jina, anwani, umri, na ujuzi wa kazi na kisha husambaza habari hizo kwa watu wengine kama vile watangazaji wa bidhaa.

      HABARI ZA SIRI NA SIMU ZA MKONONI: Hivi sasa hakuna njia ya bei nafuu ya kutunza habari za siri za watu wanaotumia simu za mkononi. Ni salama zaidi kutumia simu ya kawaida ikiwa mnazungumzia jambo la siri. Hakikisha kwamba wewe na mtu unayezungumza naye mnatumia simu za kawaida. Ujumbe kutoka kwa simu nyingi za mkononi unaweza kunaswa na redio, simu nyingine za mkononi, au hata na mashine zinazopima mpigo wa moyo wa watoto wachanga. Ukinunua bidhaa kwa kupiga simu na kutaja nambari yako ya kadi ya mkopo na tarehe yake ya mwisho, habari hizo zinaweza kuibiwa na kutumiwa vibaya na walaghai.b

      [Maelezo ya Chini]

      b Habari hii imetolewa kwenye kituo cha Internet cha shirika la Privacy Rights Clearinghouse.

  • Maoni Yanayofaa Kuhusu Faragha
    Amkeni!—2003 | Januari 22
    • Zoea la kutumia tekinolojia ya kisasa kuiba vitambulisho au kufanya ulaghai kwa kutumia habari za kibinafsi za watu wengine limeenea pia. Ni jambo la busara kuchukua hatua za kulinda habari zako za kibinafsi ili zisiwafikie watu wasiofaa.a Biblia inasema: “Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; bali wajinga huendelea mbele wakaumia.”—Mithali 22:3.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki