Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Baba Aliye Tayari Kusamehe
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 1
    • Baba katika huo mfano wenye somo wa Yesu awakilisha Mungu wetu mwenye rehema, Yehova. Sawa na mwana aliyepotea, watu fulani huacha usalama wa nyumba ya Mungu kwa wakati fulani lakini hurudi baadaye. Yehova huwaonaje? Wale ambao humrudia Yehova wakiwa wenye toba ya moyo mweupe wanaweza kuhakikishiwa kwamba “yeye hatateta sikuzote, wala hatashika hasira yake milele.” (Zaburi 103:9) Katika huo mfano wenye somo, baba alikimbia ili kumkaribisha mwana wake. Vivyo hivyo, Yehova ana nia na ana hamu ya kusamehe watenda-dhambi wenye toba. Yu “tayari kusamehe,” naye husamehe “kabisa.”—Zaburi 86:5; Isaya 55:7; Zekaria 1:3.

      Katika mfano wenye somo wa Yesu, upendo wa kweli wa baba ulifanya iwe rahisi kwa mwana kupata ujasiri wa kurudi. Lakini fikiria hili: Ni nini lingetukia ikiwa baba alikuwa amemkana huyo mvulana au katika mfoko wa hasira akamwambia asirudi kamwe? Yamkini mtazamo huo ungalimtenga mvulana huyo daima.—Linganisha 2 Wakorintho 2:6, 7.

  • Baba Aliye Tayari Kusamehe
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 1
    • Huyo baba pia alimwonyesha mwana wake huruma aliporudi. Ilimchukua muda mfupi kuona toba ya moyo mweupe ya huyo mvulana. Kisha, badala ya kusisitiza kwamba huyo mwana asimulie ukiukaji wake kinaganaga, alijishughulisha na kumkaribisha, na akaonyesha furaha kubwa katika kufanya hivyo. Wakristo wanaweza kuiga kielelezo hiki. Wapaswa kushangilia kwamba aliyepotea amepatikana.—Luka 15:10.

      Mwenendo wa baba ulionyesha wazi kwamba alitazamia kwa muda mrefu kurudi kwa mwana wake mkaidi. Bila shaka, huko kutazamia kwa baba ni kivuli tu cha tamaa ambayo Yehova anayo kwa wote ambao wameiacha nyumba yake. Yeye “hataki yeyote aangamizwe bali hutaka wote wafikie toba.” (2 Petro 3:9) Kwa hiyo wale ambao hutubu dhambi zao wanaweza kuwa na uhakika wa kwamba watabarikiwa kwa “majira ya kuburudisha . . . kutoka kwa utu wa Yehova.”—Matendo 3:19.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki