-
Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 5Amkeni!—2011 | Machi
-
-
Alipokuwa akipanua milki yake, Aleksanda pia alitimiza unabii mwingine wa Biblia. Kwa mfano, nabii Ezekieli na Zekaria, walioishi katika karne ya saba na ya sita K.W.K., walitabiri kuharibiwa kwa jiji la Tiro. (Ezekieli 26:3-5, 12; 27:32-36; Zekaria 9:3, 4) Ezekieli hata aliandika kwamba mawe yake na mavumbi yake yatawekwa “katikati ya maji.” Je, maneno hayo yalitimia?
Hebu fikiria kile ambacho majeshi ya Aleksanda yalifanya wakati yalipozingira Tiro mwaka wa 332 K.W.K. Walikwangua magofu ya jiji la bara la Tiro na kuyatupa baharini ili kutengeneza njia hadi kwenye jiji la kisiwani la Tiro. Mbinu hiyo ilifanikiwa, na Tiro likaanguka. “Unabii kuhusu Tiro, kutia ndani mambo madogo sana, ulitimizwa,” akasema mvumbuzi wa karne ya 19 wa eneo hilo.b
-
-
Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 5Amkeni!—2011 | Machi
-
-
b Kama ilivyotabiriwa na Ezekieli, Tiro lilishindwa kwa mara ya kwanza na Mfalme Nebukadreza wa Babiloni. (Ezekieli 26:7) Baadaye, jiji hilo lilijengwa upya. Jiji hilo lililojengwa upya ndilo lililoharibiwa na Aleksanda, na hivyo kutimiza maneno yote yaliyotabiriwa na manabii.
-
-
Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 5Amkeni!—2011 | Machi
-
-
[Ramani katika ukurasa wa 20]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Aleksanda alitimiza unabii wa Biblia alipotumia magofu ya jiji la zamani la bara la Tiro kujenga njia ya mawe hadi kwenye jiji la kisiwani
BARA
Njia ya mawe iliyojengwa na Aleksanda
TIRO
TIRO YA LEO
Eneo lililojazwa magofu
-