Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Biblia—Kitabu cha Unabii Sahihi, Sehemu ya 2
    Amkeni!—2012 | Juni
    • Unabii wa 2: “Kupatana na kutimia kwa miaka 70 katika Babiloni [mimi Yehova] nitawakazia ninyi fikira [Wayahudi walio uhamishoni], nami nitawatimizia neno langu jema kwa kuwarudisha tena mahali hapa [nchi ya Yuda].”—Yeremia 29:10.

      Utimizo: Baada ya miaka 70 ya uhamisho, kuanzia 607 hadi 537 K.W.K., Mfalme Koreshi wa Uajemi aliwaachilia Wayahudi waliokuwa utekwani na kuwaruhusu warudi nyumbani kwao ili wakajenge upya hekalu huko Yerusalemu.—Ezra 1:2-4.

      Historia inafunua nini?

      ● Je, Waisraeli waliendelea kuwa mateka Babiloni kwa miaka 70 kama Biblia ilivyotabiri? Hebu ona maelezo ya Ephraim Stern, ambaye ni mmoja wa wataalamu wakuu wa wachimbuaji wa vitu vya kale nchini Israel. “Kuanzia mwaka wa 604 K.W.K. hadi 538 K.W.K.—hakuna uthibitisho unaoonyesha kuwa kuna mtu aliyeishi nchini Israeli. Wakati huo, hakuna hata mji mmoja ulioharibiwa na Wababiloni unaoonekana kuwa ulikuwa na watu.” Kipindi hicho ambacho hakukuwa na mtu katika eneo lililoshindwa kinapatana sana na uhamisho wa Waisraeli kupelekwa Babiloni kuanzia 607 hadi 537 K.W.K.—2 Mambo ya Nyakati 36:20, 21.

      ● Mataifa ya kale katika eneo lote la Mesopotamia yalikuwa na kawaida ya kuandika kwenye mabamba yaliyofanyizwa kwa udongo laini. Bamba moja gumu linalojulikana kama Mwanzi wa Koreshi, linakadiriwa kuwa la mwaka wa 539 K.W.K. hivi, mwaka uleule ambao Mfalme Koreshi wa Uajemi aliipindua Milki ya Babiloni. Sehemu fulani ya maandishi hayo inasema hivi: “Mimi ni Koreshi, . . . mfalme wa Babiloni.” Maandishi hayo yanaendelea kusema hivi: “Nilirudisha kwenye majiji matakatifu [ambayo tayari yalikuwa yametajwa] yaliyokuwa upande ule mwingine wa Tigri, majengo matakatifu ambayo yamekuwa magofu kwa muda mrefu sana, [na] sanamu zilizokuwepo ndani yake . . . Mimi (pia) niliwakusanya wakazi wake wote (wa awali) na nikawarudishia makao yao.”

      Maandishi hayo yanapatana na unabii wa Biblia unaosema kwamba Wayahudi waliohamishwa wangerudishwa nyumbani kwao—unabii uliokuwa umerekodiwa miaka 200 hivi mapema.

  • Biblia—Kitabu cha Unabii Sahihi, Sehemu ya 2
    Amkeni!—2012 | Juni
    • Unabii wa 2: “Kupatana na kutimia kwa miaka 70 katika Babiloni [mimi Yehova] nitawakazia ninyi fikira [Wayahudi walio uhamishoni], nami nitawatimizia neno langu jema kwa kuwarudisha tena mahali hapa [nchi ya Yuda].”—Yeremia 29:10.

      Utimizo: Baada ya miaka 70 ya uhamisho, kuanzia 607 hadi 537 K.W.K., Mfalme Koreshi wa Uajemi aliwaachilia Wayahudi waliokuwa utekwani na kuwaruhusu warudi nyumbani kwao ili wakajenge upya hekalu huko Yerusalemu.—Ezra 1:2-4.

      Historia inafunua nini?

      ● Je, Waisraeli waliendelea kuwa mateka Babiloni kwa miaka 70 kama Biblia ilivyotabiri? Hebu ona maelezo ya Ephraim Stern, ambaye ni mmoja wa wataalamu wakuu wa wachimbuaji wa vitu vya kale nchini Israel. “Kuanzia mwaka wa 604 K.W.K. hadi 538 K.W.K.—hakuna uthibitisho unaoonyesha kuwa kuna mtu aliyeishi nchini Israeli. Wakati huo, hakuna hata mji mmoja ulioharibiwa na Wababiloni unaoonekana kuwa ulikuwa na watu.” Kipindi hicho ambacho hakukuwa na mtu katika eneo lililoshindwa kinapatana sana na uhamisho wa Waisraeli kupelekwa Babiloni kuanzia 607 hadi 537 K.W.K.—2 Mambo ya Nyakati 36:20, 21.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki