Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Tukio la Mfano” Ambalo Ni Muhimu Kwetu
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Machi 15
    • Paulo alifafanua maana ya sehemu mbalimbali za ‘tukio hilo la mfano.’ Aliandika hivi: “Wanawake hawa wanamaanisha maagano mawili, moja kutoka Mlima Sinai, ambalo huzaa watoto kwa ajili ya utumwa, na ambalo ni Hagari. . . . Naye analingana na Yerusalemu la leo, kwa maana liko katika utumwa pamoja na watoto wake.” (Wagalatia 4:24, 25) Hagari aliwakilisha Israeli halisi, ambalo jiji lake kuu lilikuwa Yerusalemu. Taifa la Wayahudi liliunganishwa na Yehova kupitia agano la Sheria lililoanzishwa kwenye Mlima Sinai. Chini ya agano la Sheria, mara kwa mara Waisraeli walikumbushwa kwamba walikuwa watumwa wa dhambi na kwamba walihitaji kukombolewa.—Yeremia 31:31, 32; Waroma 7:14-24.

  • “Tukio la Mfano” Ambalo Ni Muhimu Kwetu
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Machi 15
    • Masimulizi yaliyoongozwa kwa roho ya Mungu kuhusu matukio ya karne ya kwanza yanaonyesha kwamba taifa la kimwili lililowakilishwa na Hagari halikutokeza wana ambao wangekuwa warithi pamoja na Yesu kwa msingi wa ukoo. Wayahudi ambao waliamini kwa kiburi kwamba walikuwa na haki ya urithi huo kwa msingi wa ukoo wao walitupiliwa mbali, na wakakataliwa na Yehova. Bila shaka, baadhi ya Waisraeli wa asili walipata kuwa warithi pamoja na Kristo. Hata hivyo, walipewa pendeleo hilo kwa msingi wa imani yao katika Yesu na si kwa sababu ya ukoo wao.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki