Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mafundisho Kuhusu Kukosa Uaminifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 23. Ni nini kinachompata Shebna hatimaye, nasi twaweza kujifunza nini kutokana na hilo?

      23 Ni nini kinachompata Shebna? Hatuna rekodi yoyote juu ya jinsi unabii unaomhusu, uliorekodiwa kwenye Isaya 22:18, ulivyotimizwa. Anapojiinua mwenyewe kisha kuaibishwa, afanana na Jumuiya ya Wakristo, lakini huenda alijifunza kutokana na nidhamu hiyo. Kwa habari hiyo, yeye ni tofauti sana na Jumuiya ya Wakristo. Rabshake wa Ashuru anapotaka wakazi wa Yerusalemu wasalimu amri, msimamizi-nyumba mpya wa Hezekia, Eliakimu, aongoza wajumbe wanaoenda kumlaki. Hata hivyo, Shebna yupo pamoja naye akiwa mwandishi wa mfalme. Yaonekana kwamba Shebna angali katika utumishi wa mfalme. (Isaya 36:2, 22, kielezi-chini)

  • Mafundisho Kuhusu Kukosa Uaminifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Msimamizi-Nyumba Mwenye Ubinafsi

      16, 17. (a) Ni nani sasa anayepokea ujumbe wenye onyo kutoka kwa Yehova, na kwa nini? (b) Kwa sababu ya tamaa yake ya makuu, ni nini kitakachompata Shebna?

      16 Nabii sasa aacha kuzungumzia watu wasio waaminifu na kuanza kuzungumzia mtu mmoja asiye mwaminifu. Isaya aandika: “Bwana, BWANA wa majeshi, asema hivi, Haya! enenda kwa huyu mtunza hazina [“msimamizi-nyumba,” “NW”], yaani, Shebna, aliye juu ya nyumba, ukamwambie, Unafanyaje hapa? nawe una nani hapa? hata ukachimba kaburi hapa; ukamchimbia kaburi huko juu, na kumchongea makao katika jabali!”—Isaya 22:15, 16.

      17 Shebna ni ‘msimamizi-nyumba aliye juu ya nyumba,’ labda nyumba ya Mfalme Hezekia. Kwa hiyo, ana wadhifa mkubwa, wa pili kutoka kwa mfalme. Atarajiwa kufanya mengi. (1 Wakorintho 4:2) Ingawa hivyo, badala ya kukazia uangalifu mambo ya taifa, Shebna afuatilia utukufu wake mwenyewe. Apanga kaburi lake la anasa—kama la mfalme—lichongwe juu katika jabali. Yehova, huku akiangalia hilo, ampulizia Isaya amwonye msimamizi-nyumba huyo asiye mwaminifu: “Tazama, BWANA atakutupa kwa nguvu, kama mtu mwenye nguvu; naam, atakuzonga-zonga. Hakika atakukunja na kukutupa kama mpira, mpaka nchi iliyo mbali; huko utakufa, na magari ya utukufu wako yatakuwa kuko huko, ewe uliye aibu ya nyumba ya bwana wako. Nami nitakusukuma na kukutoa katika mahali pako, naye atakushusha utoke hapa usimamapo.” (Isaya 22:17-19) Kwa sababu ya ubinafsi wake, Shebna hatakuwa na kaburi katika Yerusalemu, hata lile la kawaida. Badala yake, atatupwa kama mpira, afe katika nchi ya mbali. Hapo pana onyo kwa wote waliokabidhiwa mamlaka miongoni mwa watu wa Mungu. Kutumia mamlaka vibaya kutasababisha kupoteza mamlaka hiyo na labda kufukuziwa mbali.

      18. Ni nani atakayechukua mahali pa Shebna, na yamaanisha nini kwamba huyo atapokea mavazi rasmi ya Shebna na ufunguo wa nyumba ya Daudi?

      18 Hata hivyo, Shebna ataondolewaje kwenye wadhifa wake? Yehova aeleza kupitia Isaya: “Itakuwa katika siku ile nitamwita mtumishi wangu Eliakimu, mwana wa Hilkia; nami nitamvika vazi lako, nitamtia nguvu kwa mshipi wako, nami nitamkabidhi yeye mamlaka yako; naye atakuwa baba kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa nyumba ya Yuda. Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.” (Isaya 22:20-22) Eliakimu, atakayechukua mahali pa Shebna, atapewa mavazi rasmi ya msimamizi-nyumba huyo pamoja na ufunguo wa nyumba ya Daudi. Biblia hufananisha “ufunguo” na mamlaka, serikali, au uwezo. (Linganisha Mathayo 16:19.) Nyakati za kale, mshauri wa mfalme, aliyekabidhiwa funguo, angeweza kusimamia kwa jumla nyumba za mfalme, hata kutoa uamuzi juu ya wale wanaoteuliwa katika utumishi wa mfalme. (Linganisha Ufunuo 3:7, 8.) Basi, ofisi ya msimamizi-nyumba ni muhimu, na yeyote anayetumikia humo hutarajiwa kufanya mengi. (Luka 12:48) Huenda Shebna anastahili, lakini kwa kuwa yeye si mwaminifu, Yehova ataweka mwingine badala yake.

      Misumari Miwili ya Mfano

      19, 20. (a) Eliakimu atathibitikaje kuwa baraka kwa watu wake? (b) Ni nini kitakachowapata wale wanaoendelea kumtegemea Shebna?

      19 Hatimaye, Yehova atumia mfano kueleza kuhamishwa kwa mamlaka kutoka kwa Shebna hadi kwa Eliakimu. Ataarifu hivi: “Nitamkaza [Eliakimu] kama msumari mahali palipo imara; naye atakuwa kiti cha utukufu kwa nyumba ya baba yake. Nao wataangika juu yake utukufu wote wa nyumba ya baba yake; wazao wake na watoto wao, kila chombo kidogo tangu vyombo vya vikombe hata vyombo vya makopo vyote pia. Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, ule msumari [Shebna] uliokazwa katika mahali palipo imara utalegea; nao utakatwa na kuanguka chini, na ule mzigo uliokuwa juu yake utakatiliwa mbali; maana BWANA amesema haya.”—Isaya 22:23-25.

      20 Katika mistari hiyo msumari wa kwanza ni Eliakimu. Atakuwa “kiti cha utukufu” kwa nyumba ya baba yake, Hilkia. Tofauti na Shebna, hataiaibisha nyumba ya baba yake wala sifa yake. Eliakimu atakuwa tegemeo lenye kudumu kwa vyombo vya nyumbani, yaani, kwa wengine walio katika utumishi wa mfalme. (2 Timotheo 2:20, 21) Kinyume chake, msumari wa pili wamrejezea Shebna. Ingawa huenda akaonekana kuwa imara, ataondolewa. Yeyote anayeendelea kumtegemea ataanguka.

      21. Nyakati za kisasa, ni nani, kama Shebna, ambaye mahali pake palichukuliwa, kwa nini palichukuliwa, na ni nani aliyepachukua?

      21 Mambo yaliyompata Shebna yatukumbusha kwamba miongoni mwa wale wanaodai kumwabudu Mungu, wale wanaokubali mapendeleo ya utumishi wapaswa kuyatumia kwa minajili ya kutumikia wengine na kumletea Yehova sifa. Hawapaswi kutumia vibaya cheo chao ili kujitajirisha au kupata umashuhuri wa kibinafsi. Kwa kielelezo, kwa muda mrefu Jumuiya ya Wakristo imejikweza yenyewe kuwa msimamizi-nyumba aliyeteuliwa, mwakilishi wa Yesu Kristo duniani. Hata hivyo, kama vile tu Shebna alivyomwaibisha baba yake kwa kutafuta utukufu wake mwenyewe, ndivyo viongozi wa Jumuiya ya Wakristo wamemletea Muumba aibu kwa kujikusanyia mali na mamlaka. Basi, wakati wa hukumu “kuanza na nyumba ya Mungu” ulipofika mwaka wa 1918, Yehova aliiondoa Jumuiya ya Wakristo. Msimamizi-nyumba mwingine aliteuliwa—“msimamizi-nyumba mwaminifu, mwenye busara”—na kuwekwa rasmi juu ya nyumba ya Yesu duniani. (1 Petro 4:17; Luka 12:42-44)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki