Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hujui Ni Wapi Itafanikiwa!
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Julai 15
    • Mfano wa Mbegu ya Haradali

      3, 4. Mfano wa mbegu ya haradali unakazia mambo gani kuhusu ujumbe wa Ufalme?

      3 Mfano wa mbegu ya haradali, ambao umeandikwa pia katika Marko sura ya 4, unakazia mambo mawili: kwanza, ukuzi mkubwa ajabu wa ujumbe wa Ufalme; pili, ulinzi ambao wale wanaokubali ujumbe huo wanapata. Yesu alisema hivi: “Tutaufananisha ufalme wa Mungu na nini, au tutauweka katika mfano gani? Kama mbegu ya haradali, ambayo ilipopandwa katika udongo ilikuwa ndiyo mbegu ndogo zaidi kuliko zote duniani—lakini baada ya kupandwa, humea na kuwa kubwa zaidi kuliko mboga nyingine zote na hutokeza matawi makubwa, hivi kwamba ndege wa mbinguni wanaweza kupata makao chini ya kivuli chake.”—Marko 4:30-32.

  • Hujui Ni Wapi Itafanikiwa!
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Julai 15
    • 8. (a) Ndege walio katika mfano wa Yesu wanawakilisha nani? (b) Hata sasa tunalindwa kutokana na nini?

      8 Yesu anasema kwamba ndege wa mbinguni wanapata makao chini ya kivuli cha Ufalme huo. Ndege hao hawawakilishi maadui wa Ufalme ambao wanajaribu kula mbegu nzuri, kama wale ndege wanaotajwa kwenye mfano wa mtu aliyetawanya mbegu katika udongo wa aina mbalimbali. (Marko 4:4) Badala yake, katika mfano huu ndege wanawakilisha watu wenye mioyo minyoofu ambao wanatafuta ulinzi ndani ya kutaniko la Kikristo. Hata sasa, watu hao wanalindwa kutokana na mazoea mapotovu na yenye kuchafua kiroho ya ulimwengu huu mwovu. (Linganisha na Isaya 32:1, 2.)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki