Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Naweza Kujilinda Jinsi Gani Shuleni?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
    • Jinsi Unavyoweza Kufanya Unaponyanyaswa Kimapenzi

      Ikiwa unanyanyaswa kimapenzi, ni jambo la kawaida kukasirika! Je, kuna jambo lolote ambalo unaweza kufanya? Kuna mengi! Fikiria mapendekezo yafuatayo.

      Kataa katakata kutongozwa. Huenda wanyanyasaji wakafikiri kwamba kusitasita kunaonyesha kwamba unakubali au huenda ukakubali, usipowasadikisha vinginevyo. Hivyo basi, siyo yako na iwe siyo. (Mathayo 5:37) Kucheka-cheka au kutenda kana kwamba unaona haya, hata ikiwa ni kwa sababu unaiona hali hiyo kuwa yenye kuaibisha, kunaweza kumfanya mnyanyasaji akuelewe vibaya. Shikilia msimamo wako na useme waziwazi. Huo ndio ulinzi bora!

      Fanya kituko. Anita anasema hivi kuhusu mtu aliyemnyanyasa: “Nililazimika kumwaibisha mbele ya marafiki wake kwa kumwambia kwa sauti kubwa AKOME kunishika-shika!” Ikawaje? “Marafiki wake wote walimcheka. Aliacha kuzungumza nami, lakini siku chache baadaye aliniomba msamaha na hata siku moja alinitetea wakati mtu mwingine alipojaribu kunisumbua.”

      Asipoacha, nenda zako. Hata ikihitajika, kimbia. Na ikiwa huwezi kukimbia, una haki ya kujilinda. (Kumbukumbu la Torati 22:25-27) Msichana mmoja Mkristo anasema, “Mvulana fulani alipojaribu kunishika kwa nguvu, nilimtwanga ngumi, na kukimbia!”

      Mwambie mtu fulani. “Hivyo ndivyo nilivyofanya mwishowe,” anasema Adrienne mwenye umri wa miaka 16. “Niliwaomba wazazi wangu mashauri nilipoanza kusumbuliwa na mvulana niliyemwona kuwa rafiki. Kadiri nilivyokataa, ndivyo alivyozidi, aliona ni mchezo tu.” Wazazi wa Adrienne walimpa mashauri mazuri yaliyomsaidia kushughulikia tatizo hilo. Bila shaka, wazazi wako pia wanaweza kukusaidia.

  • Naweza Kujilinda Jinsi Gani Shuleni?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
    • [Sanduku katika ukurasa wa 125]

      Jinsi ya Kuepuka Kunyanyaswa Kimapenzi

      Usichezee hisia za wengine. Kufanya hivyo kunaweza kuwafanya wengine waanze kukunyanyasa kimapenzi. Biblia inauliza: “Je, waweza kuweka moto kifuani na nguo zako zisiungue?” (Methali 6:27, Biblia Habari Njema) Ukweli ni kwamba, kuchezea hisia za wengine ni kucheza na moto.

      Chagua marafiki kwa hekima. Kwa kuwa waswahili hujuana kwa vilemba, huenda watu wakaamini kwamba tabia yako ni sawa na ya rafiki zako. Msichana anayeitwa Carla anasema, “Ukishirikiana na watu ambao wanapenda maneno au michezo ya kimapenzi, basi wewe pia utanyanyaswa.”—1 Wakorintho 15:33.

      Chagua mavazi kwa uangalifu. Huenda mavazi yako yakaonyesha kimakosa kwamba unataka sana kuwavutia watu wa jinsia tofauti, nawe utakuwa umechokoza nyuki.—Wagalatia 6:7.

      Wajulishe wengine kwamba wewe ni Mkristo. Usipofanya hivyo, hakuna yeyote atakayekuwa na sababu ya kutazamia uishi kulingana na viwango vya Kikristo.—Mathayo 5:15, 16.

  • Naweza Kujilinda Jinsi Gani Shuleni?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
    • [Picha katika ukurasa wa 127]

      Mwambie mtu anayekunyanyasa akome!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki