-
Ishara za Mwili na za UsoFaidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
-
-
SOMO LA 12
Ishara za Mwili na za Uso
WATU wa malezi fulani-fulani hutumia ishara zaidi kuliko watu wa malezi mengine. Lakini, karibu kila mtu hutumia ishara za uso na ishara fulani za mwili wanapoongea na watu wengine au wanapohutubia watu.
Yesu na wanafunzi wake wa mapema walizoea kutumia ishara. Pindi moja, mtu fulani alimwambia Yesu kwamba mama yake na ndugu zake wanataka kuongea naye. Yesu alijibu: “Ni nani mama yangu, na ni nani ndugu zangu?” Biblia inaendelea kusema: “Akinyoosha mkono wake kuelekea wanafunzi wake, akasema: ‘Tazama! Mama yangu na ndugu zangu!’” (Mt. 12:48, 49) Biblia inaonyesha katika Matendo 12:17 na 13:16 kwamba mtume Petro na mtume Paulo pia walitumia ishara, na kuna marejeo mengine kama hayo.
Mbali na sauti, ishara za mwili na za uso huonyesha pia mawazo na hisia. Mtu asipotumia ishara hizo vizuri, watu wanaweza kudhani hajali. Lakini mtu akitumia vizuri sauti yake pamoja na ishara, hotuba yake inakuwa bora sana. Hata kama unazungumza na mwingine kwa simu, ikiwa unatoa ishara nzuri za mwili na za uso, sauti yako itaonyesha zaidi umuhimu wa ujumbe wako na jinsi unavyohisi kuhusu jambo unalosema. Basi, kama unatoa hotuba kwa njia ya maongezi au unasoma, iwe wasikilizaji wanakuangalia au wanaangalia Biblia zao, ni muhimu kutumia ishara za mwili na za uso.
Ishara za mwili na za uso zinapasa kutokea kwa njia ya kawaida, na isionekane ni kama umeziiga kwenye kitabu. Hukujifunza jinsi ya kucheka au kuudhika.
-
-
Ishara za Mwili na za UsoFaidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
-
-
Ishara ya Uso Wako. Mara nyingi uso wako huonyesha jinsi unavyohisi kwelikweli kuliko sehemu nyingine yoyote ya mwili wako. Macho yako, umbo la mdomo wako, na kichwa chako vinahusika. Pasipo neno lolote, uso unaweza kuonyesha kutojali, machukizo, kutatanika, mshangao, au furaha. Ukionyesha ishara kama hizo unapoongea, zitakazia mambo unayosema. Muumba ameweka zaidi ya misuli 30 usoni mwako. Karibu nusu ya misuli hiyo hutumika unapotabasamu.
Iwe unatoa hotuba jukwaani au unahubiri shambani, unajaribu kuwaeleza watu ujumbe unaopendeza ambao unaweza kufurahisha mioyo yao. Tabasamu ya kutoka moyoni huthibitisha jambo hilo. Kwa upande mwingine, ikiwa uso wako hauonyeshi hisia yoyote, watu wanaweza kutia shaka kama kweli unaamini mambo unayosema.
Na zaidi, tabasamu huonyesha wengine kwamba unawapenda. Tabasamu ni muhimu sana hasa siku hizi ambapo watu huwaogopa wale wasiowafahamu. Tabasamu inaweza kuwastarehesha na kufanya watake kusikiliza zaidi.
-