-
Kuzungumza kwa njia ya kawaidaFaidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
-
-
SOMO LA 14
Kuzungumza kwa njia ya kawaida
KUONGEA kwa njia ya kawaida hufanya wengine wakuamini. Je, unaweza kuamini maneno ya mtu ambaye amefunika uso wake kwa kitu fulani? Na je, ungeamini maneno yake kama kitu hicho kinavutia kuliko sura yake halisi? Hapana. Basi uwe jinsi ulivyo kwa kawaida badala ya kuiga usemi mwingine.
Kuzungumza kwa njia ya kawaida si uzembe. Kutotumia lugha sanifu, kutamka maneno vibaya, na kutosema maneno yanayosikika wazi hakufai. Tuepuke lugha ya mtaani. Nyakati zote maneno yetu na tabia zetu ziwe na adabu. Mtu ambaye anaongea kwa njia ya kawaida haongei kwa njia rasmi kupita kiasi wala hafikirii tu kuvutia watu.
-
-
Kuzungumza kwa njia ya kawaidaFaidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
-
-
Jukwaani. Unapohutubia watu, njia bora ni kuzungumza kwa njia ya kawaida na ya maongezi. Bila shaka unahitaji kuinua sauti ikiwa wasikilizaji ni wengi. Ukiona unajaribu kukariri hotuba yako au kama una maandishi mengi mno, labda sababu ni kwamba unaogopa kukosea. Ni muhimu kutumia maneno yanayofaa, lakini maneno hayo yakizingatiwa kupita kiasi, hotuba haitapendeza wala kuvutia. Haitatokea kwa njia ya kawaida. Unapaswa kufikiria mapema kwa makini mambo ambayo utasema, lakini zingatia zaidi mawazo yako badala ya kufikiria maneno hususa utakayotumia.
Na ndivyo ilivyo unapohojiwa mkutanoni. Jitayarishe vizuri, lakini usisome wala kukariri majibu yako. Zungumza kwa njia ya kawaida ili maelezo yako yatoke moyoni na kuvutia.
Hata sifa nzuri zinaweza kuonwa na wasikilizaji kuwa si za kawaida zikitumiwa kupita kiasi. Kwa mfano, unapaswa kuzungumza kwa njia inayoeleweka wazi na kutamka maneno vizuri, au kwa njia ya kawaida. Hotuba yako inaweza kuchangamsha ukitumia vizuri ishara za kutia mkazo au za ufafanuzi, lakini ishara zinazolazimishwa au zenye kupita kiasi hukengeusha wasikilizaji. Zungumza kwa kiasi kinachofaa cha sauti lakini si kwa sauti kubwa kupita kiasi. Inafaa kuwa na shauku mara kwa mara katika hotuba, lakini epuka kuongea kwa majivuno. Ubadilifu wa sauti, shauku, na hisia zinapasa kuonyeshwa kwa njia ambayo haifanyi mtu ajielekezee fikira au kufanya wasikilizaji wawe na wasiwasi.
Watu wengine wana njia zao za kawaida za kuongea, hata wakati hawatoi hotuba. Wengine hutoa hotuba kwa njia ya maongezi zaidi. Jambo muhimu ni kuzungumza kwa njia nzuri kila siku na kujiendesha kwa njia ya Kikristo. Kisha unapotoa hotuba jukwaani, itakuwa rahisi kuongea na kutenda kwa njia ya kawaida inayopendeza.
-