Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Wakati uo huo, Sosaiti iliteua kesi mbili za kujaribia ziweze kukatiwa rufani kwa Mahakama Kuu Zaidi ya Kanada. Mojawapo ya hizo, Aimé Boucher v. His Majesty The King, ilishughulika na mashtaka ya uhaini yaliyokuwa yamefanywa mara kwa mara dhidi ya Mashahidi.

      Msingi wa kesi ya Boucher ulikuwa ile sehemu ambayo mkulima mpole aitwaye Aimé Boucher, alishiriki katika kugawanya trakti Quebec’s Burning Hate. Je, ulikuwa uhaini kujulisha juu ya jeuri ya magenge iliyoelekezwa dhidi ya Mashahidi katika Quebec, juu ya kutokujali sheria upande wa maofisa walioshughulika nao, na ithibati kwamba askofu Mkatoliki na wengine miongoni mwa makasisi Wakatoliki walikuwa wakichochea jeuri hiyo?

      Katika kuchanganua trakti iliyogawanywa, mmojawapo mahakimu wa Mahakama Kuu Zaidi alisema: “Hati hiyo ilikuwa na kichwa ‘Chuki Kuu ya Quebec kwa Mungu na Kristo na Uhuru Ni Jambo Linaloaibisha Kanada Yote;’ kwanza ilikuwa na maombi ya utulivu na kutoa sababu katika kukadiria mambo yanayoshughulikiwa katika kuunga mkono kichwa hicho; pili ilikuwa na marejezo ya ujumla kwa mnyanyaso wa kulipa kisasi uliofanywa katika Quebec juu ya Mashahidi wakiwa ndugu za Kristo; masimulizi yenye mambo mengi kuhusu visa hususa vya mnyanyaso; na mwishowe maombi kwa watu wa mkoa huo, katika kulalamika dhidi ya utawala wa magenge na mbinu za gestapo, ili kwamba, kupitia funzo la Neno la Mungu na utii kwa amri zalo, kuwe na ‘mazao mengi ya matunda mema ya upendo kwa ajili Yake na Kristo na uhuru wa kibinadamu.’”

      Uamuzi wa Mahakama ulibatilisha mashtaka ya Aimé Boucher, lakini mahakimu watatu kati ya watano waliagiza tu kesi isikizwe tena. Je, hilo lingetokeza uamuzi usio na upendeleo katika mahakama za chini? Maombi yalifanywa kupitia wakili wa Mashahidi wa Yehova ili Mahakama Kuu Zaidi yenyewe isikilize kesi hiyo tena. Kwa kushangaza, hilo lilikubaliwa. Huku maombi yakisubiri majibu, idadi ya mahakimu wa Mahakama iliongezeka, na mmojawapo mahakimu wa awali akabadili maoni yake. Tokeo katika Desemba 1950 lilikuwa ni uamuzi wa 5 dhidi ya 4, Ndugu Boucher akiondolewa mashtaka kabisa.

  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 689]

      Aimé Boucher, aachiliwa huru na Mahakama Kuu Zaidi ya Kanada katika uamuzi ambao ulifutilia mbali mashtaka ya uhaini dhidi ya Mashahidi wa Yehova

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki