Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Vita Si Yenu Bali Ni ya Mungu”
    Amkeni!—2000 | Aprili 22
    • Toka mwaka wa 1944 hadi 1946, idadi ya walioshtakiwa kwa tuhuma za kukiuka sheria za jimbo iliongezeka kutoka 40 hadi 800!

  • “Vita Si Yenu Bali Ni ya Mungu”
    Amkeni!—2000 | Aprili 22
    • Wengi walitiwa mbaroni. Idadi ya walioshtakiwa iliongezeka upesi kutoka 800 hadi 1,600. Wanasheria wengi na mahakimu walilalamika kwamba kesi za Mashahidi wa Yehova zilijaza mahakama za Quebec. Katika kujibu, tulidokeza utatuzi sahili: Acheni polisi washike wahalifu badala ya Wakristo. Kufanya hivyo kutatatua tatizo hilo!

      Wanasheria wawili Wayahudi walio jasiri, A. L. Stein wa Montreal na Sam S. Bard wa Quebec City, walitusaidia kwa kututetea katika kesi nyingi, hasa kabla sijapata kibali cha kuwa mshiriki wa baraza la wanasheria katika Quebec mnamo 1949. Pierre Elliott Trudeau, ambaye alikuja kuwa waziri mkuu wa Kanada baadaye, aliandika kwamba Mashahidi wa Yehova katika Quebec walikuwa “wamedhihakiwa, wamenyanyaswa, na kuchukiwa na jamii yetu yote, lakini wamefaulu kupambana kisheria na Kanisa, serikali, taifa, polisi, na maoni ya umma.”

      Mtazamo wa mahakama za Quebec ulidhihirishwa na jinsi ambavyo walimtendea ndugu yangu, Joe. Alishtakiwa kwa kosa la kuvuruga amani. Hakimu wa manispaa Jean Mercier alimhukumu Joe kifungo kikali cha siku 60 gerezani. Kisha, akashindwa kabisa kujizuia, akapaaza sauti akiwa kitini ya kwamba angeliweza angelimfunga Joe kifungo cha maisha gerezani!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki