Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Unaacha Yehova Akuulize Maswali?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Aprili 15
    • Yesu, yule Mwalimu Mkuu, alitumia pia maswali kwa ustadi. Vitabu vya Injili vina maswali zaidi ya 280 ambayo yaliulizwa na Yesu. Ingawa nyakati nyingine alitumia maswali kuwanyamazisha wapinzani wake, mara nyingi aliyatumia ili kugusa mioyo ya wasikilizaji wake, na kuwachochea wafikirie hali yao ya kiroho. (Mt. 22:41-46; Yoh. 14:9, 10)

  • Je, Unaacha Yehova Akuulize Maswali?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Aprili 15
    • Ingawa maswali fulani yanahitaji kujibiwa kwa sauti, mengine yanakusudiwa kumchochea mtu atafakari kwa uzito. Vitabu vya Injili vinaonyesha kwamba Yesu alitumia sana maswali yaliyowachochea watu kutafakari kwa uzito. Pindi moja, Yesu aliwaonya hivi wanafunzi wake: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode,” yaani, unafiki wao na mafundisho yao ya uwongo. (Marko 8:15; Mt. 16:12) Wanafunzi wa Yesu hawakuelewa alichomaanisha wakaanza kubishana kwa sababu walikuwa wamesahau kubeba mkate. Angalia jinsi Yesu alivyotumia maswali katika mazungumzo mafupi yaliyofuata. “Akawaambia: ‘Kwa nini mnabishana kwa sababu hamna mikate? Je, bado hamjaelewa wala kupata maana? Je, mioyo yenu ni mizito isiweze kuelewa? “Ijapokuwa mna macho, hamwoni; na ijapokuwa mna masikio, hamsikii?” . . . Je, bado hamjapata maana?’” Maswali ya Yesu yalikusudiwa kuwafanya wanafunzi wake wafikiri, na kuwachochea kutafakari kuhusu maana halisi ya maneno yake.—Marko 8:16-21.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki