Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nimethawabishwa kwa Kufanya Mabadiliko
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Desemba 15
    • Nimethawabishwa kwa Kufanya Mabadiliko

      Limesimuliwa na James A. Thompson

      Nilipozaliwa kusini mwa Marekani mnamo mwaka wa 1928, kulikuwa na sheria iliyowabagua wazungu na weusi. Kuvunja sheria hiyo kungefanya ufungwe gerezani au upewe adhabu kali zaidi.

      KATIKA sehemu fulani za Marekani wakati huo, Mashahidi wa Yehova walilazimika kuwa na makutaniko, mizunguko, na wilaya za wazungu na za weusi. Mnamo mwaka wa 1937, baba yangu akawa mtumishi wa kampuni (sasa anaitwa mratibu wa baraza la wazee) wa kutaniko la watu weusi huko Chattanooga, Tennessee. Henry Nichols alikuwa mtumishi wa kampuni wa kutaniko la watu weupe.

      Ninakumbuka mambo mazuri yaliyotukia nilipokuwa kijana. Wakati huo nilizoea kukaa nyuma ya nyumba yetu usiku nikimsikiliza Baba na Ndugu Nichols wakizungumza. Ingawa nilikuwa sielewi kila jambo walilokuwa wakizungumzia, nilifurahia kukaa karibu na Baba alipokuwa akizungumza na Ndugu Nichols kuhusu jinsi ambavyo wangeweza kutimiza vizuri kazi ya kuhubiri chini ya hali hizo.

  • Nimethawabishwa kwa Kufanya Mabadiliko
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Desemba 15
    • Nilipoingia shule ya sekondari, harakati za kutetea haki za raia zilikuwa zikipamba moto katika eneo la Kusini. Mashirika kama NAACP (Chama cha Taifa cha Maendeleo ya Watu Weusi) yaliwahimiza wanafunzi wajiunge na harakati hizo. Tulihimizwa kuwa wanachama. Shule kadhaa za watu weusi kutia ndani ile niliyosomea, ziliweka mradi wa kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanajiunga na mashirika hayo. Nilichochewa “kuunga mkono jamii yetu,” kama walivyosema. Lakini nilikataa, nikawaeleza kwamba Mungu hana ubaguzi na hapendelei jamii moja. Hivyo, ninatazamia wakati ambapo Mungu ataondoa ukosefu wowote wa haki kama huo.—Yoh. 17:14; Mdo. 10:34, 35.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki