-
Kuvuka Ukanda Mkuu wa DenmarkAmkeni!—1999 | Februari 8
-
-
Kuvuka Ukanda Mkuu wa Denmark
NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA DENMARK
TUNAPOTAZAMA Denmark kwenye ramani, tunaweza kuelewa kwa urahisi kwa nini raia wa Denmark wamekuwa mabaharia na wajenzi wa daraja kwa muda mrefu. Denmark ina visiwa 483 na peninsula inayojitokeza ndani ya bahari kutoka bara la Ulaya. Hivyo, sikuzote kusafiri kotekote katika Denmark kumehusisha kuvuka bahari.
Babu wa zamani wa Maharamia wa Skandinevia wa raia wa Denmark walijua namna ya kujenga meli zilizofaa kusafiri baharini. Na inaonekana kwamba kwa miaka mingi iliyopita, kila mji mdogo wa pwani ya Denmark umekuwa na huduma za feri zilizouunganisha na mji mwingine kwenye kisiwa jirani.
Ng’ambo ya Ukanda Mkuu
Hata hivyo, sikuzote kuvuka kwa meli kumekuwa jambo hatari. Iko hivyo unapovuka eneo pana la maji linalotenganisha visiwa viwili vikubwa zaidi vya Denmark, Sjælland na Fyn. Mlangobahari huu, Store Strait, unaenea kama ukanda mpana wa maji kutoka kaskazini hadi kusini; kwa sababu hiyo, mara nyingi unaitwa Ukanda Mkuu.
Ili kusafiri kati ya magharibi mwa Denmark na Sjælland, lilipo Copenhagen, jiji kuu la nchi, lazima uvuke Ukanda Mkuu. Zamani, hili lingemaanisha kutumia siku kadhaa ukisubiri pepo zibadili mkondo, dhoruba zitulie, au barafu ziyeyuke. Kuvuka kungechukua muda mrefu na kulikuwa hatari. Katika karne ya 16, kwa sababu ya barafu, kikundi cha kifalme kilikwama kwa muda wa juma moja kwenye kisiwa kidogo cha Sprogø, katikati ya kingo mbili.
Kwa hiyo, haishangazi kwamba wazo la kujenga daraja katika sehemu hii limewavutia raia wa Denmark kwa muda mrefu. Lakini je, daraja lolote lenye kujengwa na mwanadamu lingeweza kuvuka maji mengi yenye upana unaotoshana na Ukanda Mkuu? Lingehitaji kuwa na urefu wa kilometa 18, kutia ndani kisehemu kilichojengwa huko Sprogø. Lingefika mbali sana zaidi ya vile mtu awezavyo kuona kwa macho wakati wa halihewa ya kawaida—na ng’ambo ya bahari isiyozingirwa. Daraja la Golden Gate la San Francisco, ni lenye urefu unaopungua kilometa tatu.
Hali Yenye Kutatanisha ya Wapangaji
Kwa kweli, Bunge la Denmark lilianza kujadili suala la daraja hilo katika karne ya 19. Kwa miaka mingi iliyopita, wapangaji walihangaishwa na maswali kama haya: Je, tunataka daraja au njia ya chini kwa chini? Je, yapaswa kuunganisha magarimoshi, magari, au aina zote mbili za usafiri? Kuna ubaya gani wa kutumia feri tu?
Maelfu ya mipango ilifanywa, na maneno mengi sana yakanenwa. Usemi “mjadala wa Ukanda Mkuu” ukajulikana sana katika Denmark kukiwa na mazungumzo yasiyokoma. Lakini hatimaye, katika mwaka wa 1987, mkataa ulifikiwa. Makutano, yenye kuunganisha visiwa viwili vikubwa kwenye sehemu zao zinazokaribiana sana, yangekuwa kwa ajili ya magarimoshi na magari. Mradi huo ungehusisha madaraja mawili na njia ya chini kwa chini—muunganisho wenye umbali wa kilometa 18—pamoja uliitwa Kiungo cha Ukanda Mkuu.
-
-
Kuvuka Ukanda Mkuu wa DenmarkAmkeni!—1999 | Februari 8
-
-
Njia ya Chini kwa Chini Yenye Sehemu Mbili
Njia ya chini kwa chini, awamu ya pili ya mradi huo, ni mafanikio makubwa hasa. Njia za chini kwa chini mbili, kila moja ikiwa na kipenyo cha meta nane, zilijengwa kwa ajili ya magarimoshi. Hizo njia za chini kwa chini zilichimbwa ndani ya udongo, mawe, na matope ya maji kwa urefu wa kilometa 7.4. Na wajenzi wa njia ya chini kwa chini hawakuweza kukadiria kwa undani aina ya udongo ulio chini ya ardhi kabla ya kuanza kuchimba.
Hiyo njia ya chini kwa chini iko kati ya meta 10 na 40 chini ya bahari, ikitegemea mandhari iliyoko chini ya bahari—sehemu yenye kina zaidi ikiwa meta 75 chini ya usawa wa bahari. Kila moja ya mashine za kutoboa njia ya chini kwa chini zilizotumiwa ilikuwa na urefu wa meta zaidi ya 200, kutia ndani magarimoshi ya kuzitegemeza. Njia hizo za chini kwa chini zilizomalizika zimetandazwa kwa sehemu zilizopindwa 60,000 zilizotengenezwa kwa saruji, kila moja ikiwa na uzito upatao tani nane.
Wakianza kuchimba njia ya chini kwa chini kutoka sehemu zote mbili wakati huohuo, kwa ustadi wajenzi hao walifanikiwa kukutana katikati wakiachana kwa sentimeta nne. Lilikuwa tukio la pekee lililongojewa kwa muda mrefu wakati, katika Oktoba 15, 1994, Mkuu wa Denmark Joachim alipounganisha kirasmi nusu mbili za hiyo njia ya chini kwa chini kwa kuvuka kutoka mashine moja ya kutoboa hadi nyingine, ambayo ilikuwa ikichimba kuelekea ile ya kwanza. Kutoka Sprogø katikati ya Ukanda Mkuu, hizo njia mbili za chini kwa chini zilizokamilika sasa zinaelekea upande wa mashariki hadi pwani ya Sjælland. Tangu katikati ya mwaka wa 1997, magarimoshi huvuka kwa kasi Ukanda Mkuu yakiandaa huduma za kawaida.
-
-
Kuvuka Ukanda Mkuu wa DenmarkAmkeni!—1999 | Februari 8
-
-
Kinachomaanishwa na Kiungo Hicho
Sasa kwa kuwa jitihada za maelfu ya wapangaji na wafanyakazi zimefikia kikomo, tokeo ni gani? Bila shaka, Denmark imejipatia uvutio wa wageni, kwa kuwa madaraja hayo yanavutia kikweli unapokuwa kwenye bara au baharini. Unapokuwa ndani ya gari, hutaweza kusahau pindi uvukapo daraja lililo kubwa sana hivi kwamba mara nyingi ni vigumu kuona mwisho mmoja au miisho yote miwili! Na, bila shaka, kuvuka sasa kunachukua muda mfupi kweli. Ingawa feri ilitumia muda unaozidi saa moja, sasa garimoshi huvuka kwa kasi kwa dakika saba tu!
Kiungo hicho tayari kinabadili mazoea fulani ya watu. Raia wengi zaidi wa Denmark wanazuru marafiki, wanafanya biashara, au wanaenda kujitumbuiza ng’ambo ya bahari. Ukuzi wa miji na wa biashara unaathiriwa kwa sababu sasa inawezekana kufanya kazi upande mmoja wa ukanda huo na uwe na nyumba upande ule mwingine. Na bidhaa zaweza kusafirishwa ng’ambo ya nchi haraka zaidi ya ilivyokuwa awali.
Lakini kitu fulani pia kimepotezwa. Feri zilizosafiri mara nyingi katika bahari hii ziliwakilisha utamaduni uliodumu kwa karne kadhaa, na wasafiri wengi walipendelea kipindi cha pumziko walichopata kwa kusafiri kwa feri. Mwanabiashara mmoja alilalamika akisema hivi, “nitazikumbuka feri hizo.” “Bahari na mashua kubwa huvutia. Mimi hufurahia kupigwa na upepo ninapokuwa kwenye sitaha.” Hata hivyo, hakuna shaka kwamba kiungo hicho kipya kitaunganisha sehemu mbalimbali za ufalme wa kisiwa cha Denmark na kurahisisha usafiri wa kwenda na kutoka kaskazini mwa Ulaya.
-
-
Kuvuka Ukanda Mkuu wa DenmarkAmkeni!—1999 | Februari 8
-
-
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
DENMARK
FYN
SJÆLLAND
FYN
DARAJA LA MAGHARIBI
SPROGØ
NJIA YA CHINI KWA CHINI
DARAJA LA KUNING’INIZWA
SJÆLLAND
RELI
BARABARA KUU YA MAGARI
-