Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha Kimbingu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • na kuzunguka kiti cha ufalme kuna upinde-mvua kama emeraldi katika kuonekana.” (Ufunuo 4:3, NW)

  • Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha Kimbingu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 7. Tunaweza kujifunza nini kutokana na uhakika wa kwamba kuna upinde-mvua kuzunguka kiti cha ufalme cha Yehova?

      7 Angalia kwamba Yohana anaona kuzunguka kiti cha ufalme upinde-mvua, rangi-emeraldi chanikiwiti. Neno la Kigiriki linalotafsiriwa hapa kuwa upinde-mvua (irʹis) hudokeza umbile la duara kabisa. Upinde-mvua unatajwa kwa mara ya kwanza katika Biblia kuhusiana na siku ya Noa. Baada ya yale maji ya Gharika kutindika, Yehova alitokeza upinde-mvua katika wingu, naye akaeleza kwa maneno haya ulichofananisha: “Upinde-mvua wangu mimi natoa katika wingu, na huo lazima utumike kuwa ishara ya agano kati ya mimi na dunia. Na mimi kwa hakika nitakumbuka agano langu ambalo liko kati ya mimi na nyinyi na kila nafsi iliyo hai miongoni mwa mnofu wote; na maji hayatakuwa tena gharika kuleta mnofu wote kwenye angamio.” (Mwanzo 9:13, 15, NW) Basi, ile njozi ya kimbingu ingeleta jambo gani akilini mwa Yohana? Ule upinde-mvua alioona lazima uwe ulimkumbusha uhitaji wa uhusiano wenye amani pamoja na Yehova, kama ule unaofurahiwa na jamii ya Yohana leo. Pia ingepiga chapa akilini ule utulivu na amani ya kuwapo kwa Yehova, utulivu ambao utaenea kwa binadamu wote wenye kutii wakati Yehova atandapo hema yake juu ya aina ya binadamu katika ile jamii ya dunia mpya.—Zaburi 119:165; Wafilipi 4:7; Ufunuo 21:1-4.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki