-
Uhuru wa Kusema Je, Unatumiwa Vibaya?Amkeni!—1996 | Julai 22
-
-
Makala moja iliyokuwa katika gazeti la habari la Paris Le Figaro iliripoti kwamba kikundi cha rapu kitwacho Ministère amer (Huduma Chungu) kinahimiza mashabiki wacho kuua polisi. Mojapo mafungu ya maneno yao husema: “Hakutakuwako na amani isipokuwa [polisi] wafe.” “Kwenye muziki wetu,” akatangaza msemaji wa hicho kikundi, “twawaambia wachome vituo vya polisi na kutoa dhabihu [polisi]. Ni nini kingekuwa cha kawaida zaidi ya hicho?” Hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa dhidi ya kikundi hicho cha rapu.
Vikundi vya rapu katika Marekani pia huunga mkono uuaji wa polisi na kutangaza haki ya kusema hivyo chini ya ulinzi wa uhuru wa kusema.
-
-
Uhuru wa Kusema Nyumbani—Je, Ni Hali Itishayo Kutokeza Matatizo?Amkeni!—1996 | Julai 22
-
-
Kwa kielelezo, katika Ufaransa, wakati wanamuziki wa rapu walipopendekeza uuaji wa polisi na polisi wakauawa na watu fulani waliosikia huo muziki, je, wanamuziki hao wa rapu wangetozwa hesabu kwa kuchochea jeuri? Au wanapaswa kulindwa chini ya mswada wa haki?
-