Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Baraka au Laana—Vielelezo kwa Ajili Yetu Leo
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Juni 15
    • 13. Wakorintho wa Kwanza 10:10 laonya dhidi ya nini, na Paulo alikuwa akifikiria uasi upi?

      13 Akitaja kielelezo chake cha mwisho kilichohusisha Waisraeli jangwani, Paulo aandika hivi: “Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.” (1 Wakorintho 10:10) Uasi ulitokea wakati Kora, Dathani, Abiramu, na washiriki wao walipotenda kwa njia isiyo ya kitheokrasi wakapinga mamlaka ya Musa na Haruni. (Hesabu 16:1-3) Baada ya uharibifu wa wale waasi, Waisraeli walianza kunung’unika. Hiyo ilikuwa kwa sababu walianza kusababu kwamba uharibifu wa wale waasi haukuwa wenye haki. Hesabu 16:41 lataarifu hizi: “Siku ya pili yake mkutano wote wa wana wa Israeli wakamnung’unikia Musa, na Haruni, wakasema, Ninyi mmewaua watu wa BWANA.” Tokeo la kuchambua kwao njia ambayo haki ilitekelezwa katika pindi hiyo lilikuwa kuangamia kwa Waisraeli 14,700 kutokana na tauni iliyopelekwa kimungu.—Hesabu 16:49.

  • Baraka au Laana—Vielelezo kwa Ajili Yetu Leo
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Juni 15
    • 15 Inafaa kuuliza maswali ya moyo mweupe kuhusu habari ya Kimaandiko. Lakini namna gani ikiwa tungekuza mtazamo hasi ujionyeshao katika mazungumzo ya uchambuzi miongoni mwa kikundi cha marafiki wa karibu? Ingefaa tujiulize wenyewe, ‘Matokeo ya kunung’unika huku yaelekea kuwa nini? Je, isingefaa zaidi kuacha kunung’unika na kusali kwa unyenyekevu ili kupata hekima?’ (Yakobo 1:5-8; Yuda 17-21) Kora na wale waliomuunga mkono, walioasi dhidi ya mamlaka ya Musa na Haruni, huenda wakawa walisadikishwa sana kwamba maoni yao yalikuwa halali hivi kwamba hawakuchunguza nia zao. Hata hivyo, walikuwa wamekosea kabisa. Ndivyo na wale Waisraeli walionung’unika kuhusu uharibifu wa Kora na wale waasi wengine. Ni jambo la hekima kama nini kuruhusu vielelezo hivyo vitusukume kuchunguza nia zetu, kuondosha hali ya kunung’unika au kulalamika, na kumruhusu Yehova atutakase!—Zaburi 17:1-3.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki