Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Vijana Wengine Hupata Raha Yote?
    Amkeni!—1996 | Julai 22
    • Nyuma katika nyakati za Biblia, watu wa Mungu walifurahia utendaji mbalimbali wenye kujenga, kama vile kucheza ala za muziki, kuimba, kucheza dansi, kuzungumza, na kucheza. Pia walikuwa na pindi za kipekee kwa ajili ya ushirika wenye kusherehekea na wenye shangwe. (Yeremia 7:34; 16:9; 25:30; Luka 15:25) Kwani, Yesu Kristo mwenyewe alihudhuria sherehe ya arusi!—Yohana 2:1-10.

  • Kwa Nini Vijana Wengine Hupata Raha Yote?
    Amkeni!—1996 | Julai 22
    • Fikiria kilichotukia nyuma katika nyakati za Biblia. Waisraeli fulani walipoteza hisi yote ya usawaziko ilipohusu tafrija, wakifanya karamu zisizodhibitiwa zilizoendelea usiku kucha! Nabii Isaya alisema: “Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao.” Si kwamba lilikuwa kosa kukutana pamoja na kufurahia chakula, muziki na kucheza dansi. Lakini Isaya alisema hivi kuhusu wanakaramu hao wenye kelele: “Hawaiangalii kazi ya BWANA.”—Isaya 5:11, 12.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki