-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2011 | Desemba 1
-
-
Kochinili nyekundu, ambayo pia inaitwa kermes, ni rangi nyekundu iliyotengenezwa kutokana na wadudu fulani wa kike wa jamii ya Coccidae. Wadudu hao wasio na mabawa wanaishi kwenye aina fulani ya mti unaoitwa mwaloni (Quercus coccifera), ambao unapatikana Mashariki ya Kati na Pwani ya Mediterania. Rangi hiyo nyekundu inapatikana katika mayai yaliyo ndani ya mwili wa mdudu huyo. Anapokuwa na mayai hayo mwilini mwake, anafanana na tunda jekundu la beri. Mdudu huyo ana ukubwa na umbo kama la njugu, na hukaa kwenye majani au matawi ya mwaloni. Baada ya kuchukuliwa kwa mikono na kupondwa, wadudu hao wanatoa rangi nyekundu, ambayo inaweza kuchanganywa na maji na kutiwa kwenye kitambaa. Mwanahistoria Mroma, Plini Mkubwa, alitaja kochinili nyekundu na aliiona kuwa mojawapo ya rangi zilizothaminiwa zaidi katika siku zake.
-
-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2011 | Desemba 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 22]
Wadudu waliotumiwa kutayarisha rangi
[Hisani ya Picha]
Courtesy of SDC Colour Experience (www.sdc.org.uk)
-