-
John Foxe—Aliishi Nyakati Zenye MsukosukoAmkeni!—2011 | Novemba
-
-
John Foxe—Aliishi Nyakati Zenye Msukosuko
JE, WANADAMU hujifunza kutokana na mambo yaliyotukia wakati uliopita? Fikiria kuhusu swali hilo unapochunguza maisha ya John Foxe, Mwingereza aliyeandika kitabu akitarajia kwamba wasomaji wake wangeshutumu ukatili mbaya sana uliotukia katika nyakati zake.
Masimulizi ya John Foxe, yaliyoandikwa wakati wa yale Marekebisho Makubwa ya Kidini, yalikuwa na uvutano mkubwa juu ya watu wa Uingereza kwa karne nyingi. Kitabu chake kinachoitwa Acts and Monuments of the Church, kilichukua zaidi ya miaka 25 kukamilishwa. Na watu fulani wamesema kwamba Biblia pekee ndicho kitabu kilichokuwa na uvutano mkubwa zaidi katika lugha na utamaduni wa Waingereza.
-
-
John Foxe—Aliishi Nyakati Zenye MsukosukoAmkeni!—2011 | Novemba
-
-
Zaidi ya hilo, Foxe alianza kukusanya historia ya Lollards nchini Uingereza, na akaikamilisha mnamo 1554. Maandishi hayo yalichapishwa huko Strasbourg, ambalo leo ni jiji nchini Ufaransa, katika buku dogo la Kilatini lililofanyizwa kwa karatasi 212. Hayo yakawa maandishi yake ya kwanza katika kitabu chake kilichoitwa Acts and Monuments of the Church. Miaka mitano baadaye aliongezea sehemu nyingine kwenye kitabu hicho na mwishowe kikawa na kurasa kubwa 750.
-
-
John Foxe—Aliishi Nyakati Zenye MsukosukoAmkeni!—2011 | Novemba
-
-
Foxe Anakamilisha Kitabu Chake
Huko Uingereza, Foxe alianza kushughulikia toleo lake lililokuwa na masimulizi mengi, na huenda baadhi ya wasomaji wake walikuwa wamejionea mambo aliyoandika. Toleo lake la kwanza la Kiingereza—lililokuwa na kurasa 1,800 na michoro kadhaa iliyochongwa kwenye mbao—lilitolewa mnamo 1563, na mara moja likauzwa sana.
Toleo la pili lilitolewa miaka saba baadaye. Mabuku yake mawili, yalikuwa na zaidi ya kurasa 2,300 na michoro 153. Mwaka uliofuata, Kanisa la Anglikana liliagiza kwamba nakala ya kitabu cha Foxe iwekwe kando ya Biblia katika makanisa yote makubwa ya Uingereza na katika nyumba za wakuu wa makanisa kwa ajili ya watumishi na wageni wao. Makanisa ya parokia yakafanya vivyo hivyo pia. Hata watu ambao hawakujua kusoma na kuandika walifaidika kutokana na michoro yake, nayo ilibaki akilini mwao kwa muda mrefu.
-
-
John Foxe—Aliishi Nyakati Zenye MsukosukoAmkeni!—2011 | Novemba
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 28]
KITABU CHA WAFIA IMANI CHA FOXE
Kanisa Katoliki lilipoendelea kupigana na yale Marekebisho Makubwa ya Kidini, watu fulani barani Ulaya kama vile Jean Crespin walikuwa wakiandika kuhusu mateso na mauaji ya wafia imani nchini mwao.c Kwa sababu hiyo, kitabu cha Foxe Acts and Monuments of the Church kikaja kuitwa Kitabu cha Wafia Imani cha Foxe (Foxe’s “Book of Martyrs”). Baadaye, matoleo yaliyorekebishwa na kufupishwa yalipotolewa, kichwa hicho kilichobuniwa kikachukua mahali pa kile ambacho Foxe alichagua.
[Maelezo ya Chini]
c Ona makala “Kitabu cha Wafia Imani cha Jean Crespin” katika toleo la Machi 2011 la gazeti hili.
[Hisani ya Picha]
© Classic Vision/age fotostock
-
-
John Foxe—Aliishi Nyakati Zenye MsukosukoAmkeni!—2011 | Novemba
-
-
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 26]
From Foxe’s Book of Martyrs
-