Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matokeo ya Msiba
    Amkeni!—1996 | Agosti 22
    • Hii ndiyo hali ya mamilioni leo. Kulingana na Tume ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Wakimbizi (UNHCR), watu milioni 27 ulimwenguni pote wamekimbia vita au mnyanyaso. Watu wengine milioni 23 wamehamishwa katika nchi zao wenyewe. Yote yakiwa yamefikiriwa, mtu 1 kati ya watu 115 duniani amelazimishwa kukimbia. Walio wengi ni wanawake na watoto. Wakiwa matokeo ya vita na taabu, wakimbizi huachwa wahurumiwe na hali katika ulimwengu huu usiowataka, ulimwengu ambao huwakataa, si kwa sababu wao ni nani, bali kwa sababu ya kile walicho.

  • Idadi Yenye Kuongezeka ya Wakimbizi
    Amkeni!—1996 | Agosti 22
    • Idadi Yenye Kuongezeka ya Wakimbizi

      SEHEMU kubwa ya historia ya mwanadamu imeharibiwa na vita, njaa kuu, na mnyanyaso. Likiwa tokeo, sikuzote kumekuwa na watu wanaohitaji mahali pa kimbilio. Katika nyakati zilizopita, mataifa na watu wamepatia wale wenye uhitaji mahali pa kimbilio.

      Sheria zenye kuandaa kimbilio ziliheshimiwa na Waazteki wa kale, Waashuru, Wagiriki, Waebrania, Waislamu, na wengineo. Plato, mwanafalsafa Mgiriki, aliandika hivi zaidi ya karne 23 zilizopita: “Mgeni, akiwa ametengwa kutoka watu wa nchi yake na familia yake, apasa kuonyeshwa upendo mwingi na wanadamu na miungu. Kwa hiyo uangalifu wapasa kutolewa ili wageni wasitendewe mabaya.”

      Katika karne ya 20, idadi ya wakimbizi imeongezeka kwa kutazamisha. Katika jitihada ya kutunza wakimbizi milioni 1.5 waliobakia baada ya Vita ya Ulimwengu 2, Tume ya Umoja wa Mataifa Inayoshughulikia Wakimbizi (UNHCR) ilianzishwa katika 1951. Ilifikiriwa kwamba tume hiyo ingedumu kwa miaka mitatu, kutegemea wazo kwamba muda si muda wakimbizi waliokuwapo wangechangamana katika jamii waliyopata kimbilio. Ilifikiriwa kwamba baada ya hilo, shirika hilo lingekomeshwa.

      Hata hivyo, kwa kipindi cha miongo mingi, idadi ya wakimbizi iliongezeka sana. Kufikia 1975 idadi yao ilikuwa imefika milioni 2.4. Katika 1985 tarakimu hiyo ilikuwa milioni 10.5. Kufikia 1995 idadi ya watu wenye kupokea ulinzi na msaada kutoka kwa UNHCR ilikuwa imeongozeka kwa kutazamisha hadi milioni 27.4!

      Wengi walitumaini kwamba enzi ya baada ya Vita Baridi ingefungua njia ya kutatua tatizo la duniani pote la wakimbizi; haikulitatua. Badala ya hivyo, mataifa yamegawanyika kwa kufuata historia na ukabila, ikitokeza mapambano. Vita vilipokuwa vikiwaka, watu walitoroka, wakijua kwamba serikali zao hazingeweza kuwalinda. Kwa kielelezo katika 1991, karibu Wairaki milioni mbili walitoroka kwa idadi kubwa kuingia katika nchi za ujirani. Tangu wakati huo, wakimbizi wakadiriwao kuwa 735,000 wametoroka ile iliyokuwa Yugoslavia. Kisha, katika 1994 vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Rwanda ikalazimisha zaidi ya nusu ya watu wa nchi hiyo milioni 7.3 kutoroka makao yao. Warwanda milioni 2.1 hivi walitafuta kimbilio katika nchi za karibu za Afrika.

      Kwa Nini Tatizo Hilo Lazidi Kuwa Baya?

      Kuna sababu kadhaa ambazo zachangia idadi yenye kuongezeka ya wakimbizi. Katika mahali fulani, kama vile Afghanistan na Somalia, serikali za kitaifa zimeporomoka. Hilo limeacha mambo mikononi mwa wanamgambo wenye silaha ambao hupora nchi bila kuzuiwa, wakisababisha wasiwasi na kufanya watu watoroke.

      Mahali penginepo, mapambano husababishwa na tofauti tata sana za kikabila na kidini, kusudi kuu la vikundi vyenye kupigana likiwa kuondosha raia. Kuhusu vita katika ile iliyokuwa Yugoslavia, mwakilishi wa UM aliomboleza hivi katikati mwa 1995: “Kwa watu wengi ni vigumu sana kufahamu visababishi vya vita hii: ni nani anayepigana, sababu za kupigana. Watu wengi mno wanatoka upande mmoja na kisha majuma matatu baadaye watu wengi wanatoka upande ule mwingine. Ni vigumu sana kufahamu hata kwa watu ambao eti wanafahamu.”

      Silaha za kisasa haribifu mno—roketi zenye kurushwa kwa mfuatano, makombora, mizinga, na silaha kama hizo—huongezea machinjo na kupanua mweneo wa mapambano. Tokeo: wakimbizi wengi hata zaidi. Katika nyakati za hivi majuzi asilimia 80 hivi ya wakimbizi wa ulimwenguni imetoroka kutoka nchi zenye kuendelea hadi nchi za ujirani ambazo zinaendelea pia na zisizo na vifaa vya kutunza wale wanaotafuta kimbilio.

      Katika mapambano mengi ukosefu wa chakula huchangia tatizo hilo. Watu wanapokufa njaa, labda kwa sababu msafara wa ugavi wa kutuliza wazuiwa, watu walazimika kuhama. Gazeti The New York Times lataja: “Katika mahali kama vile Pembe ya Afrika, ukame na vilevile vita vimeharibu bara hilo hivi kwamba haliwezi kuandaa riziki tena. Iwe hayo mamia ya maelfu yanatoroka kufa njaa au vita si jambo la maana.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki