Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kupata Makao ya Kudumu
    Amkeni!—2002 | Januari 22
    • Maelfu ya watu walifika mpakani. Lakini kwa kuwa katika miaka ya karibuni wakimbizi milioni moja walikuwa tayari wameingia katika nchi hiyo jirani, haikukubali wakimbizi wengine. Mapolisi wa mpakani wenye marungu, waliwazuia watu wasivuke mpaka.

      Afisa mmoja wa uhamiaji katika eneo hilo alitaja wazi sababu za kuwazuia wakimbizi hao wasiingie nchini humo. Alisema hivi: “Hawalipi kodi. Wao huharibu barabara. Wao hukata miti. Wao humaliza maji. La, hatutaki wakimbizi wengine.”a

      Matukio hayo ya kuhuzunisha yameongezeka sana. Watu waliolazimishwa kuhama hukabili ugumu wa kupata makao ya kudumu. Ripoti moja ya hivi majuzi ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International ilisema hivi: ‘Idadi ya wakimbizi inapoongezeka, nchi mbalimbali zinakataa hata zaidi kuwasaidia.’

  • Kupata Makao ya Kudumu
    Amkeni!—2002 | Januari 22
    • Huenda serikali za nchi zinazoendelea, ambazo hukumbwa na maelfu ya wakimbizi kwa ghafula, tayari zinashindwa kulisha raia zake. Serikali hizo haziwezi kuwasaidia sana wakimbizi wote wanaotaka kuingia katika nchi zao. Na kwa kuwa mataifa tajiri yana matatizo yao yenyewe, yanaweza kusita kuwasaidia wakimbizi walio katika nchi nyingine.

  • Kupata Makao ya Kudumu
    Amkeni!—2002 | Januari 22
    • Huenda wenyeji pia wakaumia kwa sababu ya ongezeko kubwa la wakimbizi wenye njaa. Katika eneo la Maziwa Makuu ya Afrika, maafisa fulani walilalamika hivi: “[Wakimbizi] wameharibu maghala yetu, mashamba yetu, mifugo yetu, mbuga zetu, wamesababisha njaa na kueneza magonjwa . . . [Wao] hupata misaada ya chakula lakini sisi hatupati chochote.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki