-
Ukristo Ukitenda Katikati ya MsukosukoMnara wa Mlinzi—1998 | Januari 15
-
-
“Hata hivyo, ndugu kutoka Ulaya walileta fedha zilizotuwezesha kununua chakula, kilichokuwa adimu na ghali sana. Hicho chakula kilikuja wakati wa maana sana, kwa kuwa wengi hawakuwa na chakula chochote nyumbani mwao. Tuligawanya hicho chakula kwa Mashahidi na wasio Mashahidi. Ikiwa huo msaada haukuja wakati ambapo ulikuja, wengi zaidi wangalikufa, hasa watoto. Yehova aliwaokoa watu wake. Wasio Mashahidi walivutiwa sana. Wengi wao walieleza juu ya muungano na upendo wetu. Baadhi yao walikiri kwamba dini yetu ndiyo ya kweli.”
-
-
Ukristo Ukitenda Katikati ya MsukosukoMnara wa Mlinzi—1998 | Januari 15
-
-
Msaada kwa Wasio Mashahidi
Msaada huo wa huruma haukupewa Mashahidi wa Yehova pekee. Wengine pia walinufaika, kama vile wengi walivyonufaika mwaka wa 1994. Hilo lapatana na andiko la Wagalatia 6:10, ambalo lataarifu hivi: “Basi, kwa kweli maadamu tuna wakati wenye kufaa kwa ajili ya hilo, acheni sisi tufanye lililo jema kuelekea wote, lakini hasa kuelekea wale ambao katika imani ni jamaa zetu.”
Mashahidi waligawa dawa na mavazi kwenye shule kadhaa za msingi na makao ya watoto yatima karibu na Goma. Hayo makao ya watoto yatima ni nyumba ya watoto 85. Katika safari ya mapema zaidi ya kuchunguza hali, kikoa cha kutoa msaada kilizuru hayo makao ya watoto yatima na kuahidi kuwaletea ugavi wa masanduku 50 ya biskuti zenye kiwango cha juu cha protini, masanduku ya mavazi, mablanketi 100, dawa, na vichezeo. Hao watoto walipanga laini katika ua na kuwaimbia hao wageni. Kisha wakatoa ombi la pekee—je, wangeweza kuwa na mpira hivi kwamba wangeweza kucheza soka?
Majuma kadhaa baadaye hicho kikoa cha kutoa msaada kilitimiza ahadi zao za kuleta ugavi. Akiwa amevutiwa na ukarimu na yale aliyokuwa amesoma katika fasihi za Biblia alizokuwa amepewa, mkurugenzi wa hayo makao ya watoto yatima alisema kwamba alikuwa akielekea kuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Na je, hao watoto walipewa mpira? “La,” akajibu Claude, msimamizi wa kikoa cha kutoa msaada kutoka Ufaransa. “Tuliwapa mipira miwili.”
-