Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kitu Kisichoweza Kuharibiwa na Dhoruba
    Amkeni!—2003 | Agosti 8
    • Kisha walianza kuwasaidia watu walioishi katika ujirani. Mtu mmoja mwenye mkahawa karibu na Jumba la Ufalme alifurahi sana Mashahidi walipoondoa takataka na matope kutoka katika vyumba vyake vya chini ya ardhi na ghorofa ya chini.

  • Kitu Kisichoweza Kuharibiwa na Dhoruba
    Amkeni!—2003 | Agosti 8
    • Frank na Elfriede, wenzi wa ndoa ambao ni Mashahidi, walifanya kazi pamoja na majirani wao kwa siku kadhaa kabla ya furiko. Walijaza magunia kwa mchanga na kuyapanga kwenye kingo za mto ili kuziimarisha. Baada ya maji kupungua Frank na Elfriede waliwatembelea watu walioathiriwa na furiko hilo ili kuwapelekea chakula na kuwafariji. Frank anasema hivi: “Bibi mmoja hakuweza kuamini kwamba wageni walimletea chakula bila kutoza malipo. Alituambia kwamba hakuna yeyote wa kanisa lake aliyekuwa amemtembelea. Na lile shirika lililokuwa limemletea chakula lilikuwa limetoza malipo kwa kila mlo. Watu walishangaa kuwaona Mashahidi wa Yehova wakija na chakula motomoto badala ya vitabu vya Biblia.”

  • Kitu Kisichoweza Kuharibiwa na Dhoruba
    Amkeni!—2003 | Agosti 8
    • Pia wengi ambao si Mashahidi walisaidiwa. Kwa mfano, mwanamke mmoja alivutiwa sana Shahidi mmoja alipokuja nyumbani kwake saa moja na nusu asubuhi na kumwuliza ikiwa anahitaji msaada. Ilimbidi mwanamke huyo ahame kwa sababu tayari maji yalikuwa yakiingia katika nyumba yake. Hata hivyo, aliporudi, alipata barua ndogo kutoka kwa Mashahidi hao kwenye lango la bustani yake. Barua hiyo ilisema hivi: “Ukihitaji msaada, tuite mara moja.” Mashahidi walisaidia kuondoa takataka na matope kutoka katika nyumba na bustani yake.

      Mashahidi 100 walikwenda hadi mji wa Au ili kuwasaidia Mashahidi wa huko na majirani wao. Wale walioongoza kazi hiyo walitembelea wakazi wa eneo hilo na kuwauliza ikiwa wangehitaji msaada. Watu walishangaa kuwaona Mashahidi wakija na vyombo vya kuondoa maji na vya usafi, kama vile pampu za kusukuma maji, fagio, na vyombo vya kuchimbia. Kazi ambayo ingaliwachukua wenye nyumba juma zima kumaliza, ilimalizika kwa saa chache tu. Watu walitazama wakitokwa na machozi.

  • Kitu Kisichoweza Kuharibiwa na Dhoruba
    Amkeni!—2003 | Agosti 8
    • Mwanamke mmoja alisema hivi: “Ningalifurahi kama kanisa langu lingalitoa msaada kama nyinyi Mashahidi.” Mwanamke mwingine aliyesaidiwa na Mashahidi alisema hivi: “Mashahidi wa Yehova waliokoa maisha yetu. Kwa upendo walihatarisha maisha yao ili kutuokoa nyumba yetu ilipofurikwa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki