-
“Fuliza Kushikilia kwa Imara Kile Ulicho Nacho”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Mlango Uliofunguliwa”
18. Ni kuweka rasmi gani alikofanya Yesu katika 1919, na hivyo mwekwa alikuwaje kama mtumishi wa nyumba mwaminifu wa Hezekia?
18 Katika 1919 Yesu alitimiza ahadi yake na kukitambua kile kikosi kidogo cha Wakristo wapakwa-mafuta cha kweli kuwa “mtumwa mwaminifu mwenye akili” wake. (Mathayo 24:45-47) Hao waliingia ndani ya pendeleo linalofanana na lile alilofurahia Eliakimu mtumishi wa nyumba mwaminifu katika wakati wa Hezekia.d Yehova alisema hivi kwa habari ya Eliakimu: “Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.” Eliakimu alibeba begani madaraka mazito kwa ajili ya Hezekia, yule mwana wa kifalme wa Daudi. Hali moja na hiyo leo, jamii ya Yohana ya wapakwa-mafuta imewekelewa begani mwayo “ufunguo wa nyumba ya Daudi” katika maana ya kwamba wameaminishwa masilahi ya kidunia ya Ufalme wa Kimesiya. Yehova ameimarisha watumishi wake kwa ajili ya pendeleo hili, akiongezea nguvu chache zao kuwa nishati yenye msukumo inayotosha kwa ushuhuda mkubwa wa tufe lote.—Isaya 22:20, 22; 40:29.
19. Jamii ya Yohana ilishughulikiaje madaraka ambayo ilipewa na Yesu katika 1919, kukiwa na tokeo gani?
19 Tangu 1919 na kuendelea mabaki ya wapakwa-mafuta, wakifuata kielelezo cha Yesu, walianzisha kampeni yenye bidii ya kutangaza kotekote habari njema za Ufalme. (Mathayo 4:17; Warumi 10:18)
-
-
“Fuliza Kushikilia kwa Imara Kile Ulicho Nacho”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Chati katika ukurasa wa 64]
Katika 1919 yule Mfalme anayetawala Yesu alifungua mlango wa nafasi kwa utumishi wa Kikristo. Nambari yenye kuongezeka ya Wakristo waliojitoa wametumia kwa faida nafasi hiyo.
Mabara Wakristo Wahubiri
Yaliyofikiwa Walioshiriki wa Wakati
1918 14 3,868 591
1928 32 23,988 1,883
1938 52 47,143 4,112
1948 96 230,532 8,994
1958 175 717,088 23,772
1968 200 1,155,826 63,871
1978 205 2,086,698 115,389
1988 212 3,430,926 455,561
1998 233 5,544,059 698,781
2005 235 6,390,022 843,234
[Maelezo ya Chini]
e Tarakimu zilizo juu ni wastani wa kila mwezi.
f Tarakimu zilizo juu ni wastani wa kila mwezi.
[Picha katika ukurasa wa 65]
Utendaji wa Mashahidi wa Yehova unatolewa kwa moyo mzima wote. Mathalani, fikiria zile saa ambazo wametumia katika kuhubiri na kufundisha na ile hesabu kubwa mno ya mafunzo ya Biblia bila malipo ambayo wameongoza katika nyumba za watu.
Saa Zilizotumiwa Mafunzo ya Biblia
Kuhubiri Yaliyoongozwa
Mwaka (Jumla ya Mwaka) (Wastani wa Mwezi)
1918 19,116 Hayakurekodiwa
1928 2,866,164 Hayakurekodiwa
1938 10,572,086 Hayakurekodiwa
1948 49,832,205 130,281
1958 110,390,944 508,320
1968 208,666,762 977,503
1978 307,272,262 1,257,084
1988 785,521,697 3,237,160
1998 1,186,666,708 4,302,852
2005 1,278,235,504 6,061,534
-