Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ole wa Pili—Majeshi ya Wapanda-Farasi
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na malaika wa sita akapuliza tarumbeta yake. Na mimi nikasikia sauti moja kutoka pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu ikisema kwa malaika wa sita, ambaye alikuwa na tarumbeta: ‘Fungua malaika wanne ambao wamefungwa kwenye mto mkubwa Eufrati.’” (Ufunuo 9:13, 14, NW)

  • Ole wa Pili—Majeshi ya Wapanda-Farasi
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 3. Ni jinsi gani malaika wanne walikuwa “wamefungwa kwenye mto mkubwa Eufrati”?

      3 Ni jinsi gani malaika hao walikuwa “wamefungwa kwenye mto mkubwa Eufrati”? Katika nyakati za kale mto Eufrati ulikuwa ndio mpaka wa kaskazini-mashariki wa lile bara ambalo Yehova alikuwa amemwahidi Abrahamu. (Mwanzo 15:18; Kumbukumbu 11:24) Kwa wazi, hao “malaika” walikuwa wamezuiliwa mpakani mwa bara lao walilopewa na Mungu, au milki ya kidunia ya utendaji, wakizuiwa wasiingie kabisa ndani ya utumishi ambao Yehova alikuwa amewatayarishia. Pia Eufrati ulikuwa umeshirikishwa sana na lile jiji la Babuloni, na baada ya anguko la Yerusalemu katika 607 K.W.K., Waisraeli wa mnofu walitumia miaka 70 huko katika utekwa, ‘wakiwa wamefungwa kwenye mto mkubwa Eufrati.’ (Zaburi 137:1) Mwaka wa 1919 uliwapata Waisraeli wa kiroho wakiwa wamefungwa katika kizuizi kama hicho, wakiwa wamehuzunika na wakiomba Yehova wapate mwongozo.

      4. Ni utume gani ambao malaika wanne wanao, na umetimizwaje?

      4 Kwa furaha, Yohana anaweza kuripoti: “Na wale malaika wanne walifunguliwa, ambao wametayarishwa kwa ajili ya saa na siku na mwezi na mwaka, kuua theluthi ya wanadamu.” (Ufunuo 9:15, NW) Yehova ni Mtunza-Wakati aliye sahihi. Yeye ana ratiba ya wakati naye anashikamana nayo. Kwa sababu hiyo, wajumbe hawa wanaachiliwa barabara kulingana na ratiba na kwa wakati ili watimize kazi waliyo nayo kufanya. Wazia shangwe yao walipotoka kwenye utumwa katika 1919, wakiwa tayari kwa kazi!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki