-
Wokovu Unahitajiwa!Mnara wa Mlinzi—2008 | Machi 1
-
-
Wokovu Unahitajiwa!
KWA ghafula, maji mengi sana yalifurika katika mgodi mmoja wa makaa ya mawe karibu na Pittsburgh, Pennsylvania, Marekani. Wachimba-migodi tisa walikwama mita 73 chini ya ardhi katika sehemu ndogo yenye hewa. Siku tatu baadaye, walitoka ndani ya mgodi huo wakiwa salama salimini. Waliokolewa jinsi gani?
Wakitumia ramani za mgodi huo na Mfumo wa Kupokea Habari Kutoka kwa Setilaiti, waokoaji walichimba shimo lenye upana wa sentimita 65 na kuwateremshia kifaa cha kuwaokolea. Wachimba-migodi hao waliokolewa mmoja baada ya mwingine kutoka katika mgodi huo ambao ungekuwa kaburi lao. Wote walifurahi na kushukuru sana baada ya kuokolewa.
-
-
Wokovu Unahitajiwa!Mnara wa Mlinzi—2008 | Machi 1
-
-
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]
Photo by Gene J. Puskar-Pool/Getty Images
-