-
Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Azimio la 1922 lilikuwa na kichwa “Mwito kwa Viongozi wa Ulimwengu”—naam, wito wathibitishe dai lao la kwamba wangeweza kuleta amani, ufanisi, na furaha kwa ajili ya wanadamu au, wakishindwa, wakiri kwamba ni Ufalme wa Mungu ulio mikononi mwa Mesiya wake uwezao kutimiza mambo hayo. Katika Ujerumani, azimio hilo lilipelekwa kwa posta kwa maliki Mjerumani aliyekuwa uhamishoni, kwa rais, na kwa washiriki wote wa Bunge la Ujerumani; na nakala milioni nne unusu hivi zikapelekewa umma. Katika Afrika Kusini, Edwin Scott, akibeba mgongoni fasihi zilizokuwa katika mfuko na bakora ikiwa mkononi mwake ili kufukuza mbwa wakali, alitembelea miji 64, akigawanya binafsi nakala 50,000. Baadaye, wakati makasisi Waholanzi katika Afrika Kusini walipotembelea makao ya washiriki wa parishi wao ili kukusanya michango, wengi wao walitikisa azimio hilo usoni pa makasisi na kusema: “Yawapasa msome hili nanyi hamngekuja tena kupata pesa kutoka kwetu.”
-
-
Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Picha katika ukurasa wa 427]
Edwin Scott, katika Afrika Kusini, aligawanya yeye binafsi nakala 50,000 za “Mwito kwa Viongozi wa Ulimwengu”
-