-
‘Nafsi Zilizochinjwa’ ZathawabishwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na joho jeupe lilipewa kwa kila mmoja wao; na wao waliambiwa wapumzike kwa kitambo kidogo zaidi, mpaka hesabu ilipokuwa imejazwa pia ya watumwa wenzao na ndugu zao ambao walikuwa karibu kuuawa kama wao pia walivyokuwa.” (Ufunuo 6:11, NW)
-
-
‘Nafsi Zilizochinjwa’ ZathawabishwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
12. Ni katika njia gani Wakristo waliofufuliwa ‘hupumzika kwa kitambo kidogo zaidi,’ na mpaka lini?
12 Ithibati yote huonyesha kwamba ufufuo huu wa kimbingu ulianza katika 1918, baada ya Yesu kuketishwa juu ya kiti cha ufalme katika 1914 na kutoka kwake aende akipanda farasi kuanza ushindi wake wa kifalme kwa kuzisafisha mbingu watoke Shetani na roho waovu wake. Hata hivyo, wapakwa-mafuta hao waliofufuliwa wanaambiwa kwamba lazima “wapumzike kwa kitambo kidogo zaidi, mpaka hesabu . . . pia ya watumwa wenzao” ijazwe. Wale wa jamii ya Yohana ambao wangali duniani lazima wathibitishe ukamilifu wao chini ya jaribu na mnyanyaso, na huenda baadhi ya hawa bado wakauawa. Hata hivyo, mwishowe, damu yote yenye uadilifu iliyomwagwa na Babuloni Mkubwa na hawara zake wa kisiasa italipiwa kisasi. Kwa wakati uliopo, pasipo shaka wale waliofufuliwa wana shughuli wakiwa na wajibu mwingi wa kimbingu. Wao wanapumzika, si kwa kustarehe katika raha ya kutotenda, bali katika njia ya kwamba wao wanangojea kwa subira siku ya kisasi cha Yehova. (Isaya 34:8; Warumi 12:19) Pumziko lao litakwisha wakati wao watashuhudia uharibifu wa dini bandia na, wakiwa ‘walioitwa na waliochaguliwa na waaminifu,’ wao wanaandamana na Bwana Yesu Kristo katika kutekeleza hukumu hapa duniani juu ya sehemu nyingine zote za mbegu mbovu ya Shetani.—Ufunuo 2:26, 27; 17:14; Warumi 16:20.
-