Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Watu Wa Mungu Warudi Nchini Kwao
    ‘Ona Nchi Nzuri’
    • Kupatana na sera hiyo, Koreshi aliwaruhusu Wayahudi warudi kwao na kuanzisha tena ibada ya kweli na kujenga Yerusalemu, kama inavyoelezwa na Ezra na Nehemia. Unafikiri kundi hilo kubwa la watu walipitia wapi walipokuwa wakirudi kwao? Je, walitumia njia aliyotumia Abrahamu kwa kupitia upande wa juu wa Mto Efrati hadi Karkemishi au labda walitumia njia fupi zaidi kupitia Tadmori na Damasko? Biblia haielezi jambo hilo. (Ona ukurasa wa 6-7.)

  • Watu Wa Mungu Warudi Nchini Kwao
    ‘Ona Nchi Nzuri’
    • [Sanduku katika ukurasa wa 25]

      Chini ya utawala wa Zerubabeli, wanaume Waisraeli wapatao 50,000 walisafiri umbali wa kati ya kilometa 800 hadi 1,600 (ikitegemea njia waliyopitia) kurudi Yerusalemu. Walikabili hali ngumu sana ya kiuchumi. Nchi yao ilikuwa imeachwa ukiwa kwa miaka 70. Waisraeli waliorudi walianza kurudisha ibada ya kweli kwa kujenga madhabahu na kumtolea Yehova dhabihu. Katika mwezi wa Oktoba, mwaka wa 537 K.W.K., walisherehekea Sikukuu ya Vibanda. (Yer 25:11; 29:10) Kisha Waisraeli hao wakaweka msingi wa nyumba ya Yehova.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki