Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nuru kwa Mataifa
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 9. Yehova anatangaza habari njema zipi?

      9 Je, kuharibiwa kwa Yerusalemu mwaka wa 607 K.W.K. kunamaanisha kwamba Yehova hatakuwa tena na mashahidi duniani? Sivyo. Watu walio na uaminifu-maadili wenye kutokeza, kama vile Danieli na waandamani wake watatu, wataendelea kumtumikia Yehova hata wakiwa wahamishwa Babiloni. (Danieli 1:6, 7) Naam, ule mfuatano wa mashahidi wengi waaminifu wa Yehova utabaki hivyo hivyo, na mwishoni mwa miaka 70, wanaume na wanawake waaminifu wataondoka Babiloni kurudi Yuda ili kuirudisha ibada safi huko. Hilo ndilo jambo ambalo sasa Yehova anagusia: “Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa.”—Isaya 66:19.

      10. (a) Wayahudi waaminifu waliokombolewa Babiloni watakuwaje ishara? (b) Ni nani leo wanaokuwa ishara?

      10 Kundi la wanaume na wanawake waaminifu wanaorudi Yerusalemu mwaka wa 537 K.W.K. litatumika likiwa ishara ya kugutusha, ushuhuda wa kwamba Yehova amewakomboa watu wake. Ni nani angaliwaza kwamba siku moja Wayahudi mateka wangekuwa huru ili kufuatia ibada safi kwenye hekalu la Yehova?

  • Nuru kwa Mataifa
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 11. (a) Baada ya kurudishwa, itakuwaje kwamba watu wa mataifa watakuja kujifunza habari za Yehova? (b) Andiko la Zekaria 8:23 lilitimizwaje mara ya kwanza?

      11 Lakini, baada ya kurudishwa mwaka wa 537 K.W.K., watu wa mataifa ambao hawajawahi kuisikia habari za Yehova watamjuaje? Si Wayahudi wote waaminifu watakaorudi Yerusalemu mwishoni mwa utekwa wa Kibabiloni. Wengine, kama vile Danieli, watabaki Babiloni. Na wengine zaidi watatawanyika hadi pembe nne za dunia. Kufikia karne ya tano K.W.K., sehemu zote za Milki ya Uajemi zilikuwa na Wayahudi. (Esta 1:1; 3:8) Bila shaka wengine wao waliwaeleza majirani zao wapagani habari za Yehova, kwa maana wengi kutoka mataifa hayo walikuja kuwa waongofu Wayahudi. Inaonekana hata yule towashi Mwethiopia aliyehubiriwa na Filipo mwanafunzi Mkristo katika karne ya kwanza alikuwa mwongofu. (Matendo 8:26-40) Yote hayo yalitukia yakiwa utimizo wa kwanza wa maneno ya nabii Zekaria: “Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.” (Zekaria 8:23) Kwa kweli, Yehova aliyapelekea mataifa nuru!—Zaburi 43:3.

      ‘Kumletea Yehova Zawadi’

      12, 13. Kuanzia mwaka wa 537 K.W.K., “ndugu” wataletwa Yerusalemu kwa njia gani?

      12 Baada ya Yerusalemu kujengwa upya, Wayahudi waliotawanyika mbali sana na nchi yao wataelekeza fikira na mtazamo wao kwenye jiji hilo pamoja na ukuhani wake uliorudishwa likiwa kituo cha ibada safi. Wengi wao watasafiri mbali kuhudhuria sherehe za kila mwaka huko. Isaya anaandika hivi kwa kupuliziwa: “Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka [“zawadi,” “NW”] kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka [“zawadi,” “NW”] yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi. Na baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani na Walawi.”—Isaya 66:20, 21.

      13 Wengine wa hao ‘ndugu kutoka mataifa yote’ walikuwako siku ya Pentekoste wakati roho takatifu ilipomiminwa juu ya wanafunzi wa Yesu. Masimulizi hayo yanasema hivi: “Kulikuwa na Wayahudi wakikaa katika Yerusalemu, wanaume wenye kumhofu Mungu, kutoka kila taifa la yale yaliyo chini ya mbingu.” (Matendo 2:5) Walikuja Yerusalemu kuabudu kulingana na desturi ya Kiyahudi, lakini walipozisikia habari njema juu ya Yesu Kristo, wengi walionyesha wazi kwamba wanamwamini kisha wakabatizwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki