-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Ahadi Yenye Kufariji
3, 4. (a) Isaya aandika maneno gani yenye faraja ambayo watu wa Mungu watayahitaji baadaye? (b) Kwa nini wakazi wa Yuda na Yerusalemu watapelekwa uhamishoni huko Babiloni, na utumwa wao utadumu muda gani?
3 Katika karne ya nane K.W.K., nabii Isaya aandika maneno yenye faraja ambayo watu wa Yehova watayahitaji baadaye. Mara baada ya kumwambia Mfalme Hezekia kuhusu uharibifu unaokaribia wa Yerusalemu na kuhamishwa kwa Wayahudi hadi Babiloni, Isaya aandika maneno ya Yehova yenye ahadi ya kurudishwa: “Watulizeni [“wafarijini,” “BHN”] mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.”—Isaya 40:1, 2.
4 Neno “wafarijini,” lililo mwanzoni mwa Isaya sura ya 40, lafafanua vema ujumbe wa nuru na wa tumaini ulio katika sehemu nyinginezo za kitabu cha Isaya. Wakazi wa Yuda na Yerusalemu watapelekwa uhamishoni huko Babiloni mwaka wa 607 K.W.K. kwa sababu wameasi. Ingawa hivyo, mateka hao Wayahudi hawatawatumikia Wababiloni milele. Utumwa wao utadumu tu hadi uovu wao ‘uachiliwe.’ Itachukua muda mrefu kadiri gani? Nabii Yeremia asema ni miaka 70. (Yeremia 25:11, 12) Baadaye, Yehova atawaongoza mabaki wenye kutubu warudi Yerusalemu kutoka Babiloni. Katika mwaka wa 70 wa ukiwa wa Yuda, yafariji kama nini mateka hao kufahamu kwamba wakati wa ukombozi wao ulioahidiwa umekaribia!—Danieli 9:1, 2.
5, 6. (a) Kwa nini safari ndefu ya kutoka Babiloni hadi Yerusalemu haitazuia utimizo wa ahadi ya Mungu? (b) Kurudishwa kwa Wayahudi nchini kwao kutayaathirije mataifa mengine?
5 Safari ya kutoka Babiloni hadi Yerusalemu ni kilometa 800 hadi 1,600, ikitegemea njia inayopitiwa. Je, safari hiyo ndefu itazuia kutimia kwa ahadi ya Mungu? Hata kidogo! Isaya aandika: “Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA [“Yehova,” “NW”]; nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, na kila mlima na kilima kitashushwa; palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patasawazishwa; na utukufu wa BWANA utafunuliwa, na wote wenye mwili watauona pamoja; kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.”—Isaya 40:3-5.
6 Kabla ya kuanza safari, mara nyingi watawala wa Mashariki wangetuma watu kuitengeneza njia kwa kuondoa mawe makubwa na hata kujenga madaraja na kusawazisha vilima. Kwa Wayahudi wanaorudi, itakuwa kana kwamba Mungu mwenyewe yuko mstari wa mbele, akiondoa vikwazo vyovyote vile. Kwani, hao ni watu wa jina la Yehova, na kutimiza ahadi yake ya kuwarudisha nchini kwao kutafanya utukufu wake udhihirike mbele ya mataifa yote. Yapende yasipende, mataifa hayo yatalazimika kutambua kwamba Yehova ndiye Mtimizaji wa ahadi zake.
-
-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
8 Hata hivyo, namna gani wale wanaotazamia kunufaika na utimizo wa kwanza wa ahadi hiyo—mateka Wayahudi huko Babiloni? Je, kweli waweza kuitumainia ahadi ya Yehova ya kuwarudisha katika nchi yao wanayoipenda? Ndiyo kabisa! Kupitia maneno na vielezi vyenye kusisimua vinavyotokana na maisha ya kila siku, Isaya sasa atoa sababu madhubuti zinazoonyesha kwa nini wawe na tumaini kamili kwamba Yehova atalitimiza neno lake.
Mungu Ambaye Neno Lake Hudumu Milele
9, 10. Isaya atofautishaje ufupi wa uhai wa mwanadamu na kudumu kwa “neno” la Mungu?
9 Kwanza, neno la Yule anayeahidi kurudishwa hudumu milele. Isaya aandika: “Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani, na wema wake wote ni kama ua la kondeni; majani yakauka, ua lanyauka; kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani. Majani yakauka, ua lanyauka; bali neno la Mungu wetu litasimama [“ladumu,” “BHN”] milele.”—Isaya 40:6-8.
10 Waisraeli wafahamu vema kuwa majani hayadumu milele. Katika msimu wa ukame, joto kali la jua huyabadili kutoka kijani hadi kuwa rangi ya kahawia iliyoparara. Kwa njia fulani, uhai wa mwanadamu ni kama majani, ni wa muda mfupi sana. (Zaburi 103:15, 16; Yakobo 1:10, 11) Isaya atofautisha ufupi wa uhai wa mwanadamu na kudumu kwa “neno” la Mungu, au kusudi lake lililotaarifiwa. Naam, “neno la Mungu wetu” hudumu milele. Mungu asemapo, hakuna kiwezacho kuyabatilisha maneno yake wala kuyazuia yasitimie.—Yoshua 23:14.
-
-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Mungu Mwenye Nguvu Anayetunza Kondoo Zake kwa Wororo
12, 13. (a) Kwa nini ahadi ya kurudishwa yaweza kutumainiwa? (b) Kuna habari gani njema kwa wahamishwa Wayahudi, na kwa nini wanaweza kuwa na uhakika?
12 Isaya atoa sababu ya pili ya kuitumaini ahadi ya kurudishwa. Anayeahidi ni Mungu mwenye nguvu anayewatunza watu wake kwa wororo. Isaya aendelea: “Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, panda juu ya mlima mrefu; wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, paza sauti kwa nguvu; paza sauti yako, usiogope; iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu. Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa [“na nguvu,” “NW,” kielezi-chini], na mkono wake ndio utakaomtawalia; tazameni, thawabu yake i pamoja naye, na ijara yake i mbele zake. Atalilisha kundi lake kama mchungaji, atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; na kuwachukua kifuani mwake, nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.”—Isaya 40:9-11, chapa ya 1989.
13 Katika nyakati za Biblia, wanawake walikuwa na desturi ya kusherehekea ushindi, wakipaza sauti au wakiimba habari njema za mapigano waliyoshinda au za kitulizo kinachokuja. (1 Samweli 18:6, 7; Zaburi 68:11) Isaya aonyesha kwa unabii kwamba kuna habari njema kwa wahamishwa Wayahudi, habari zinazoweza kutangazwa kwa sauti kubwa bila hofu, hata kwenye vilele vya milima—Yehova atawaongoza watu wake kurudi kwenye jiji wanalolipenda, Yerusalemu! Wanaweza kuwa na uhakika, kwa kuwa Yehova atakuja “na nguvu.” Basi hakuna kiwezacho kumzuia asitimize ahadi yake.
14. (a) Isaya atoaje kielezi cha jinsi ambavyo Yehova atawaongoza watu wake kwa wororo? (b) Ni kielelezo gani kinachoonyesha jinsi ambavyo wachungaji hutunza kondoo zao kwa wororo? (Ona sanduku kwenye ukurasa wa 405.)
14 Hata hivyo, Mungu huyu mwenye nguvu ana sifa ya wororo. Isaya aeleza kwa uchangamfu jinsi Yehova atakavyowaongoza watu wake kurudi nchini kwao. Yehova ni kama mchungaji mwenye upendo anayewakusanya pamoja wana-kondoo wake na kuwabeba “kifuani” mwake. Yaonekana neno hili “kifua” larejezea mikunjo ya juu ya vazi. Nyakati nyingine wachungaji hubebea kifuani wana-kondoo waliozaliwa hivi karibuni ambao hawauwezi mwendo wa kundi. (2 Samweli 12:3) Onyesho kama hilo lenye kuvutia linalotokana na maisha ya uchungaji hapana shaka lawapa tena watu wa Yehova waliohamishwa uhakikishio wa utunzaji wake wenye upendo kwao. Kwa hakika Mungu huyo mwenye nguvu lakini mwenye wororo aweza kutumainiwa atimize yale ambayo amewaahidi!
-