-
“Jina Jipya”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
‘Yehova Amekufurahia’
9. Eleza jinsi hali ya Sayuni inavyogeuzwa.
9 Upaji wa jina jipya ni sehemu ya kumgeuza Sayuni wa kimbingu, anayewakilishwa na watoto wake wa kidunia, ili awe na hali ya kupendeza. Tunasoma hivi: “Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba [Namfurahia]; na nchi yako Beula [Ameolewa]; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa.” (Isaya 62:4) Sayuni wa kidunia amekuwa ukiwa tangu alipoharibiwa mwaka wa 607 K.W.K. Hata hivyo, maneno ya Yehova yanamhakikishia kwamba nchi yake itarudishiwa hali yake ya kwanza na kujazwa wakaaji tena. Sayuni aliyeteketezwa wakati mmoja hatakuwa tena mwanamke aliyeachwa pweke, wala nchi yake haitakuwa ukiwa tena. Kurudishwa kwa Yerusalemu mwaka wa 537 K.W.K. kunamaanisha kwamba atapata hali mpya, inayotofautiana kabisa na hali yake ya kwanza ya kuwa magofu. Yehova anatangaza kwamba Sayuni ataitwa “Namfurahia,” na nchi yake itaitwa “Ameolewa.”—Isaya 54:1, 5, 6; 66:8; Yeremia 23:5-8; 30:17; Wagalatia 4:27-31.
-
-
“Jina Jipya”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
11. Wayahudi wanamwoaje mama yao?
11 Yehova anazidi kukazia hali mpya ya kukubalika kwa watu wake, anapotangaza hivi: “Kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amafurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.” (Isaya 62:5) Wayahudi, wale “wana” wa Sayuni, wanawezaje kumwoa mama yao? Katika maana ya kwamba wana wa Sayuni wanaorudi baada ya kufunguliwa watoke uhamishoni Babiloni wanamiliki jiji lao kuu la zamani na kukaa humo tena. Inapokuwa hivyo, Sayuni si mkiwa tena, bali ana wana chungu nzima.—Yeremia 3:14.
-
-
“Jina Jipya”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
“Msiwe na Kimya”
13, 14. (a) Nyakati za kale, Yerusalemu linakuwaje jiji lenye usalama? (b) Nyakati za kisasa, Sayuni amekuwaje “sifa duniani”?
13 Jina jipya la mfano ambalo Yehova amewapa watu wake huwafanya wahisi usalama. Wanajua kwamba yeye huwakubali na kwamba wao ni miliki yake. Sasa Yehova anatumia mfano tofauti na kuongea na watu wake kana kwamba anaongea na jiji lenye kuta: “Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha [“kumtaja,” “NW”] BWANA, msiwe na kimya; wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.” (Isaya 62:6, 7) Katika wakati wa Yehova, baada ya mabaki waaminifu kutoka Babiloni, Yerusalemu linakuwa “sifa duniani”—jiji lenye kuta za kuwapa wakaaji wake usalama. Mchana na usiku, walinzi katika kuta hizo wako macho kuhakikisha kwamba jiji lina usalama, na kuwapasha wakaaji wake habari za kuwaonya.—Nehemia 6:15; 7:3; Isaya 52:8.
-
-
“Jina Jipya”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Kutumikia Mungu Kutathawabishwa
17, 18. (a) Wakaaji wa Sayuni wanaweza kutazamiaje kufurahia matunda ya kazi yao? (b) Watu wa Yehova leo wanafurahiaje matunda ya kazi yao?
17 Jina jipya ambalo Yehova anawapa watu wake linawahakikishia kwamba jitihada zao si za bure. “BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi. Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.” (Isaya 62:8, 9) Mkono wa kuume wa Yehova na mkono wa nguvu zake ni ishara za kuonyesha uwezo wake na nguvu zake. (Kumbukumbu la Torati 32:40; Ezekieli 20:5) Anapoapa kwa mkono wake wa kuume na kwa mkono wa nguvu zake, hiyo inaonyesha kwamba amepiga moyo konde kuibadili hali ya Sayuni. Mwaka wa 607 K.W.K., Yehova anaruhusu adui za Sayuni wamnyang’anye mali zake na kuzipora. (Kumbukumbu la Torati 28:33, 51) Lakini sasa, mali za Sayuni zitafurahiwa na wale tu walio na haki ya kuzigusa.—Kumbukumbu la Torati 14:22-27.
-
-
“Jina Jipya”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
19, 20. (a) Vikwazo vinaondolewaje njiani ili Wayahudi warudi Yerusalemu? (b) Katika nyakati za kisasa, vikwazo vimeondolewaje njiani ili watu watiifu waingie katika tengenezo la Yehova?
19 Vilevile lile jina jipya linafanya tengenezo la Yehova liwavutie watu wenye mioyo ya kupenda haki. Makundi ya watu yanalimiminikia, na njia inaachwa wazi ili waendelee kuingia. Unabii wa Isaya unasema hivi: “Piteni, piteni, katika malango; itengenezeni njia ya watu; tutieni, tutieni barabara [“kuu,” “NW”]; toeni mawe yake; twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu.” (Isaya 62:10) Katika kisa cha kwanza, inaelekea kuwa mwito huu unamaanisha kupita na kutoka nje ya malango ya jiji ya Babilonia ili kurudi Yerusalemu. Hao wenye kurudi wanapaswa kuondoa mawe njiani ili kurahisisha safari na kuinua ishara ya kuonyesha njia ya kupitia.—Isaya 11:12.
-
-
“Jina Jipya”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
21, 22. Yehova amesimamisha ishara gani ili iwaongoze wale wanaotoka katika dini ya uwongo, nasi tunajuaje?
21 Mwaka wa 537 K.W.K., jiji la Yerusalemu likawa ishara iliyowavutia mabaki Wayahudi ili warudi wakajenge hekalu upya. (Isaya 49:22)
-
-
“Jina Jipya”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
“Wokovu Wako Unakuja”!
23, 24. Wale walio na imani katika Mungu wanaletewaje wokovu?
23 Jina jipya ambalo Yehova anapatia tengenezo lake lililo kama mke linahusiana na wokovu wa milele wa watoto wake. Isaya anaandika hivi: “Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; tazama, thawabu yake i pamoja naye, na malipo yake yako mbele zake.” (Isaya 62:11) Wokovu uliwajia Wayahudi wakati Babiloni ilipoanguka, nao wakarudia nchi yao. Lakini maneno haya yanaelekeza kwenye jambo kubwa zaidi. Tangazo la Yehova linatokeza kikumbusha cha unabii huu wa Zekaria unaohusu Yerusalemu: “Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; tazama, mfalme wako anakuja kwako; ni mwenye haki, naye ana wokovu; ni mnyenyekevu, amepanda punda, naam, mwana-punda, mtoto wa punda.”—Zekaria 9:9.
24 Miaka mitatu na nusu baada ya Yesu kubatizwa katika maji na kutiwa mafuta kwa roho ya Mungu, alipanda punda akaingia Yerusalemu na kulisafisha hekalu la jiji hilo. (Mathayo 21:1-5; Yohana 12:14-16)
-