-
Misherehekeo ya Matukio Muhimu Katika Historia ya IsraeliMnara wa Mlinzi—1998 | Machi 1
-
-
Baada ya Uhamisho
14. Ni nini kilichoongoza kwenye msherehekeo wa tukio muhimu katika mwaka wa 537 K.W.K.?
14 Baada ya kifo cha Yosia, hilo taifa liligeukia tena ibada isiyo ya kweli, yenye kushusha. Mwishowe, mwaka wa 607 K.W.K., Yehova aliadhibu watu wake kwa kuyaleta majeshi ya Babiloni dhidi ya Yerusalemu. Hilo jiji na hekalu lake liliharibiwa na nchi ikaachwa ukiwa. Ilifuata miaka 70 ya utekwa wa Wayahudi katika Babiloni. Kisha Mungu akahuisha mabaki ya Wayahudi wenye kutubu, waliorudi kwenye Bara Lililoahidiwa ili kurudisha upya ibada ya kweli. Waliwasili kwenye jiji lililoangamizwa la Yerusalemu mwezi wa saba wa mwaka wa 537 K.W.K. Jambo la kwanza walilofanya lilikuwa kujenga madhabahu ili kutoa dhabihu za kila siku kama ilivyoonyeshwa katika agano la Sheria. Jambo hilo lilifanywa wakati uliofaa kabisa kwa ajili ya msherehekeo mwingine wa kihistoria. “Wakaishika Sikukuu ya Vibanda, kama ilivyoandikwa.”—Ezra 3:1-4.
-
-
Misherehekeo ya Matukio Muhimu Katika Historia ya IsraeliMnara wa Mlinzi—1998 | Machi 1
-
-
17, 18. (a) Ni msherehekeo gani wa tukio muhimu uliofikiwa mwaka wa 455 K.W.K.? (b) Tukoje katika hali kama hiyo leo?
17 Miaka 60 baadaye, mwaka wa 455 K.W.K., tukio jingine muhimu lilifikiwa. Mwaka huo Msherehekeo wa Vibanda ulitia alama ukamilisho wa kujengwa upya kwa kuta za Yerusalemu. Biblia yaripoti hivi: “Mkutano wote wa watu, waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, wakafanyiza vibanda, wakakaa katika vibanda hivyo; maana tokea siku za Yoshua, mwana wa Nuni, hata siku ile, wana wa Israeli hawakufanya hivyo. Pakawa na furaha kubwa sana.”—Nehemia 8:17.
-