-
Ikiwa Muumba Anajali, Mbona Wanadamu Wanateseka Sana?Je, Kuna Muumba Anayekujali?
-
-
Muumba ana uwezo wa kumsaidia mtu ambaye aliteseka na kufa—akimrudisha kwenye uhai, akimfufua.
Lazaro ni mtu ambaye alifufuliwa. (Yohana 11:17-45; ona ukurasa wa 158-160.) Profesa Donald MacKay alitumia mfano wa faili ya kompyuta. Aliandika kwamba kuharibika kwa kompyuta si lazima kumaanishe kwamba hesabu iliyokuwa ndani yake imeharibika. Hesabu iyo hiyo inaweza kuwekwa katika kompyuta mpya na iendelee kutumika “ikiwa mtaalamu wa hesabu anataka.” Profesa MacKay aliendelea kusema: “Inaonekana kwamba sayansi ya utendaji wa ubongo haiwezi kupinga tumaini la uhai wa milele linalotajwa katika [Biblia], ambalo kwa kawaida hukazia ‘ufufuo.’” Mwanadamu akifa, Muumba baadaye anaweza kumfufua, kama alivyomfufua Yesu na kama Yesu alivyomfufua Lazaro. MacKay alikata kauli kwamba kifo cha mtu hakiwezi kuzuia kufufuliwa kwake katika mwili mpya “ikiwa Muumba wetu anataka.”
Ndiyo, ni Muumba aliye na utatuzi wa mwisho. Ni yeye pekee awezaye kuondoa kuteseka, madhara ya dhambi, na hata kifo. Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake juu ya tukio lenye kutokeza ambalo lingali mbele yetu. Alisema: “Saa inakuja ambayo katika hiyo wote wale waliomo ndani ya makaburi ya ukumbusho watasikia sauti yake na kutoka.”—Yohana 5:28, 29.
Ebu fikiria! Mtawala Mwenye Enzi Kuu ya ulimwengu yuko tayari naye anaweza kufufua wale wote walio katika kumbukumbu yake. Hawa watapewa fursa ya kujithibitisha kuwa wenye kustahili kupokea “uhai ulio halisi.”—1 Timotheo 6:19; Matendo 24:15.
-
-
Ikiwa Muumba Anajali, Mbona Wanadamu Wanateseka Sana?Je, Kuna Muumba Anayekujali?
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 181]
Je, Ufufuo wa Mtu Wawezekana?
Mtaalamu wa ubongo Richard M. Restak alieleza juu ya ubongo wa wanadamu na miunganisho yake. “Kila kitu kuhusu mtu na kila kitu ambacho tumefanya kinaweza kujulikana na mtazamaji awezaye kusoma miunganisho ya [ubongo] na utendaji ambao umewekwa katika chembe zetu bilioni 50 za neva.” Ikiwa ndivyo hali ilivyo, je, Muumba wetu mwenye upendo hawezi kujenga upya mtu kwa kutumia habari alizo nazo kuhusu mtu huyo?
-
-
Ikiwa Muumba Anajali, Mbona Wanadamu Wanateseka Sana?Je, Kuna Muumba Anayekujali?
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 182]
Miunganisho Yako ya Ubongo Imehesabiwa
Yesu alisema: “Nywele zenyewe za kichwa chenu zimehesabiwa zote.” (Mathayo 10:29-31) Vipi ubongo? Chembe za ubongo ni ndogo-ndogo sana hivi kwamba zinaweza kuonekana tu kwa kutumia darubini kali sana. Ebu wazia kujaribu kuhesabu, si tu chembe za ubongo, bali ile miunganisho midogo sana, ambayo huweza kufikia 250,000 katika chembe fulani za ubongo.
Dakt. Peter Huttenlocher, akitumia darubini kali ya elektroni, alikuwa wa kwanza kuhesabu miunganisho ya chembe za ubongo ya watu waliokufa—za vijusu, za watoto waliokufa, na za watu wazee. Kwa kushangaza, kwa kila sampuli, kila moja ikitoshana na kichwa cha pini, zote zilikuwa na karibu idadi sawa ya chembe za ubongo, 70,000 hivi.
Kisha Dakt. Huttenlocher akaanza kuhesabu miunganisho katika chembe za ubongo, kwenye sampuli hizo zinazotoshana na vichwa vya pini. Chembe za ubongo wa kile kijusi zilikuwa na miunganisho milioni 124; zile za mtoto aliyetoka tu kuzaliwa zilikuwa na milioni 253; na mtoto wa miezi minane alikuwa na milioni 572. Dakt. Huttenlocher alipata kwamba baadaye, mtoto alipoendelea kukua, idadi hiyo ilipungua polepole.
Ugunduzi huo unapendeza kwa kufikiria yale ambayo Biblia inasema juu ya ufufuo. (Yohana 5:28, 29) Ubongo wote wa mtu mzima una karibu bilioni milioni moja ya miunganisho, yaani, 1 ikifuatwa na sufuri 15. Je, Muumba ana uwezo wa kuhesabu hiyo miunganisho na hata wa kuijenga upya?
Kitabu The World Book Encyclopedia chasema kwamba katika ulimwengu kuna nyota bilioni mara bilioni 200, au 2 ikifuatiwa na sufuri 20. Muumba ajua nyota hizo zote kwa majina. (Isaya 40:26) Basi, yeye anaweza kukumbuka na kujenga upya miunganisho ya chembe za ubongo ambayo hufanyiza kumbukumbu na hisia za wanadamu ambao anachagua kuwafufua.
-