-
Je, Uliwahi Kuishi Katika Mwili Mwingine?Mnara wa Mlinzi—2012 | Desemba 1
-
-
Ufufuo—Tumaini Lililothibitishwa kwa Ajili ya Wafu
Biblia ina masimulizi manane kuhusu watu waliojionea wafu wakifufuliwa hapa duniani.b Masimulizi hayo yanataja watu hao walifufuliwa wala si kubadilika na kuwa na mwili mwingine. Watu wa ukoo na marafiki waliwatambua watu wao waliofufuliwa. Watu hao wa ukoo hawakuhitaji kutafuta kati ya watoto waliokuwa wamezaliwa hapo karibu na kuchagua yupi kati yao alikuwa na nafsi ya mtu wao aliyekuwa amekufa.—Yohana 11:43-45.
-
-
Je, Uliwahi Kuishi Katika Mwili Mwingine?Mnara wa Mlinzi—2012 | Desemba 1
-
-
b Masimulizi hayo manane yanapatikana katika 1 Wafalme 17:17-24; 2 Wafalme 4:32-37; 13:20, 21; Luka 7:11-17; 8:40-56; Yohana 11:38-44; Matendo 9:36-42; 20:7-12. Unaposoma masimulizi hayo, ona jinsi ufufuo huo ulivyofanywa mbele ya watu wengi waliojionea. Simulizi la tisa linaeleza kuhusu kufufuliwa kwa Yesu Kristo.—Yohana 20:1-18.
-