Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uwezo wa Kurudisha Hali Nzuri—Yehova ‘Anafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya’
    Mkaribie Yehova
    • 18 Hebu wazia jambo lililotukia siku za Eliya. Mjane mmoja alikuwa amebeba mwili wa mwanaye pekee. Mvulana huyo alikuwa mfu. Haikosi jambo hilo lilimshtua nabii Eliya, aliyekuwa ameishi katika nyumba ya mjane huyo kwa muda fulani. Mapema, alimwokoa mtoto huyo asife njaa. Yaelekea Eliya alimpenda sana mvulana huyo. Mamaye alihuzunika sana. Mvulana huyo pekee ndiye aliyemfanya amkumbuke mume wake aliyekuwa amekufa. Huenda alitumaini kwamba mwanaye angemtunza akizeeka. Mjane huyo aliyefadhaika alidhani kwamba labda alikuwa akiadhibiwa kwa sababu ya dhambi fulani aliyotenda zamani. Eliya hakuweza kuvumilia msiba huo wenye kusikitisha sana. Alitwaa huyo mfu kwa upole kutoka katika kifua cha mamaye, akampeleka katika chumba chake orofani, kisha akamwomba Yehova Mungu arudishe nafsi au uhai, wa mtoto huyo.—1 Wafalme 17:8-21.

  • Uwezo wa Kurudisha Hali Nzuri—Yehova ‘Anafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya’
    Mkaribie Yehova
    • Mjane akimpokea kwa furaha mwana wake aliyefufuliwa na nabii Eliya

      “Tazama, mwanao yu hai”!

      Hata hivyo, katika kisa cha Eliya, mwana wa mjane tayari alikuwa amekufa—lakini si kwa muda mrefu. Yehova alimthawabisha nabii huyo mwenye imani kwa kumfufua mwana huyo! Kisha Eliya akamrudisha mvulana huyo kwa mamaye, akanena maneno haya yasiyoweza kusahaulika: “Tazama, mwanao yu hai”!—1 Wafalme 17:22-24.

      21, 22. (a) Ufufuo mbalimbali unaosimuliwa katika Maandiko ulikuwa na kusudi gani? (b) Ni watu wangapi watakaofufuliwa katika Paradiso, na ni nani atakayewafufua?

      21 Hivyo basi, kwa mara ya kwanza kabisa katika Biblia, twaona Yehova akitumia uwezo wake wa kuwafufua wanadamu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki