Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ndani ya Chumba Kilichofungwa
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
    • Yesu aliyefufuliwa awatokea mitume wake

      HADITHI YA 103

      Ndani ya Chumba Kilichofungwa

      BAADA ya Petro na Yohana kuondoka kwenye kaburi la Yesu, Mariamu anabaki hapo peke yake. Aanza kulia. Ndipo anainama na kuchungulia kaburi, kama ulivyoona picha ya mwisho. Anawaona malaika humo! Wanamwuliza: ‘Kwa nini unalia?’

      Mariamu ajibu: ‘Wamemchukua Bwana wangu, sijui walikomweka.’ Ndipo Mariamu ageuka na kuona mwanamume. Anamwuliza: ‘Unamtafuta nani?’

      Mariamu anadhani mwanamume huyo anatunza bustani, na labda amechukua mwili wa Yesu. Basi anamwambia hivi: ‘Ikiwa umemchukua, niambie ulipomweka.’ Kumbe huyo ndiye Yesu. Amevaa mwili ambao Mariamu hatambui. Lakini anapomwita jina lake, Mariamu anajua ni Yesu. Anakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi hivi: ‘Nimemwona Bwana!’

      Baadaye siku hiyo, wanafunzi wawili wanapotembea kwenye kijiji cha Emau, mtu fulani anajiunga nao. Wanapoendelea njiani, mtu huyo anawaeleza mambo mengi ya kufurahisha kutoka Biblia. Mwishowe, wanapoanza kula, wanafunzi hao wanatambua kwamba mtu huyo ni Yesu. Kisha Yesu anaacha kuonekana, na upesi wanafunzi hao wawili wanarudi Yerusalemu kwenda kuwaambia mitume habari zake.

      Hayo yanapoendelea, Yesu anajionyesha tena kwa Petro. Wengine wanapopata habari hizo wanafurahi. Ndipo wanafunzi hao wawili wanakwenda Yerusalemu na kuwakuta mitume. Wanawaambia namna Yesu alivyowatokea pia njiani. Wakati wanaposema hayo, unajua ajabu inayotokea?

      Ebu itazame picha. Yesu atokea mle mle chumbani, ijapo mlango umefungwa kwa kufuli. Wanafunzi wanafurahi! Je! hiyo si siku ya furaha? Unaweza kuhesabu mara ambazo Yesu sasa ameonekana kwa wafuasi wake? Unahesabu mara tano?

      Mtume Tomaso (Tomasi) hayuko nao wakati Yesu anapoonekana. Basi wanafunzi wanamwambia: ‘Tumemwona Bwana!’ Lakini Tomaso hawezi kusadiki mpaka ajionee mwenyewe Yesu. Basi, siku nane zikiisha kupita wanafunzi wanakusanyika tena katika chumba kilichofungwa, wakati huu Tomaso yuko nao. Mara moja, Yesu atokea mle mle chumbani. Tomaso anasadiki sasa.

      Yohana 20:11-29; Luka 24:13-43.

  • Yesu Anarudi Mbinguni
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
    • Mitume  wanaangalia wakati Yesu anapaa kwenda mbinguni

      HADITHI YA 104

      Yesu Anarudi Mbinguni

      WAKATI siku zinapopita, Yesu anajionyesha kwa wafuasi wake mara nyingi. Wakati mmoja wanafunzi kama 500 wanamwona. Anapowatokea, unajua Yesu anawaambia nini? Ufalme wa Mungu. Yehova alimtuma Yesu duniani afundishe habari za Ufalme huo. Anazidi kufanya hivyo hata baada ya kufufuliwa katika wafu.

      Unakumbuka maana ya ufalme wa Mungu? Ufalme ni serikali halisi ya Mungu mbinguni, naye Yesu Ndiye Mungu amechagua awe mfalme. Kama tulivyokwisha jifunza, Yesu alionyesha atakavyokuwa mfalme mwema sana kwa kulisha wenye njaa chakula, kwa kuponya wagonjwa, hata kufufua wafu!

      Basi, Yesu atakapotawala mbinguni kwa miaka elfu, dunia itakuwaje? Dunia yote itafanywa kuwa paradiso nzuri. Hakutakuwako vita tena, wala uvunjaji wa sheria, wala magonjwa, wala hata kifo. Twajua hayo ni ya kweli kwa sababu Mungu aliifanya dunia iwe paradiso watu wafurahie. Ndiyo maana aliifanya bustani ya Edeni mwanzoni. Naye Yesu atatimiza mapenzi ya Mungu.

      Sasa wafika wakati wa Yesu kurudi mbinguni. Kwa muda wa siku 40 amekuwa akijionyesha kwa wanafunzi wake. Basi wana hakika kwamba yuko hai tena. Lakini kabla ya kuacha wanafunzi wake anawaambia hivi: ‘Kaeni Yerusalemu mpaka mpokee roho takatifu.’ Roho takatifu ni nguvu ya utendaji ya Mungu, ni kama upepo unaovuma, itakayosaidia wafuasi wake wafanye mapenzi ya Mungu. Mwishowe, anasema: ‘Mtahubiri habari zangu kwenye sehemu za mbali za dunia.’

      Yesu akiisha kusema hivyo, ajabu yatokea. Anaanza kupanda mbinguni, kama unavyoona hapa. Ndipo wingu lamficha asionekane, na wanafunzi hawamwoni Yesu tena.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki