Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kifo Kitafanywa Kuwa Si Kitu”
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Julai 1
    • Ni Nani Wanaofufuliwa?

      13. Ni ono gani la ufufuo linalorekodiwa kwenye Ufunuo 20:12-14?

      13 Ono la Yohana juu ya ufufuo wa kidunia limerekodiwa kwenye Ufunuo 20:12-14 hivi: “Nikaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha ufalme, na hati-kunjo zikafunguliwa. Lakini hati-kunjo nyingine ikafunguliwa; hiyo ndiyo hati-kunjo ya uhai. Na hao wafu wakahukumiwa kutokana na mambo yale yaliyoandikwa katika hizo hati-kunjo kulingana na vitendo vyao. Nayo bahari ikawatoa hao wafu waliokuwa ndani yayo, na kifo na Hadesi vikawatoa wafu ndani yavyo, nao walihukumiwa mmoja-mmoja kulingana na vitendo vyao. Na kifo na Hadesi vikavurumishwa ndani ya ziwa la moto. Hili humaanisha kifo cha pili, ziwa la moto.”

  • “Kifo Kitafanywa Kuwa Si Kitu”
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Julai 1
    • 15. Yamaanisha nini kusema kwamba wanaofufuliwa “[watahukumiwa] kutokana na mambo yale yaliyoandikwa katika hizo hati-kunjo”?

      15 Wenye kufufuliwa “[watahukumiwaje] kutokana na mambo yale yaliyoandikwa katika hizo hati-kunjo kulingana na vitendo vyao”? Hati-kunjo hizo si rekodi ya vitendo vyao vya wakati uliopita; walipokufa, waliondolewa hatia ya dhambi walizofanya maishani mwao. (Waroma 6:7, 23) Hata hivyo, wanadamu wenye kufufuliwa bado watakuwa chini ya dhambi ya Kiadamu. Basi, ni lazima iwe kwamba hati-kunjo hizo zitaeleza kikamili maagizo ya kimungu ambayo wote lazima wafuate ili wanufaike kikamili na dhabihu ya Yesu Kristo. Alama ya mwisho ya dhambi ya Kiadamu inapofutwa, “kifo kitafanywa kuwa si kitu” katika maana kamili. Kufikia mwisho wa miaka elfu, Mungu “[ata]kuwa vitu vyote kwa kila mtu.” (1 Wakorintho 15:28) Mwanadamu hatahitaji tena uingiliaji-kati wa Kuhani wa Cheo cha Juu au Mfidi. Wanadamu wote watarudishwa kwenye hali ya ukamilifu ambayo Adamu alifurahia hapo awali.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki