-
Je, Uliwahi Kuishi Katika Mwili Mwingine?Mnara wa Mlinzi—2012 | Desemba 1
-
-
Ufufuo—Tumaini Lililothibitishwa kwa Ajili ya Wafu
Biblia ina masimulizi manane kuhusu watu waliojionea wafu wakifufuliwa hapa duniani.b Masimulizi hayo yanataja watu hao walifufuliwa wala si kubadilika na kuwa na mwili mwingine. Watu wa ukoo na marafiki waliwatambua watu wao waliofufuliwa. Watu hao wa ukoo hawakuhitaji kutafuta kati ya watoto waliokuwa wamezaliwa hapo karibu na kuchagua yupi kati yao alikuwa na nafsi ya mtu wao aliyekuwa amekufa.—Yohana 11:43-45.
Jambo lenye kufariji ni kwamba Neno la Mungu linaonyesha kuwa watu wengi ambao wamekufa watafufuliwa wakati Mungu atakapowafufua watu katika ulimwengu mpya, ambao hivi karibuni utachukua mahali pa ulimwengu huu mwovu. (2 Petro 3:13, 14) Wakati huu, mtindo wa maisha wa mabilioni ya watu umehifadhiwa katika kumbukumbu kamilifu la Yehova ambalo halina kipimo, Mungu ambaye anakumbuka majina ya nyota zote! (Zaburi 147:4; Ufunuo 20:13) Atakapomaliza kuwarudishia watu wengi uhai katika ulimwengu mpya, watakuwa na uwezo wa kufuatilia ukoo wao na kutambua mababu zao. Hilo ni tumaini lenye kuvutia kama nini!
-