-
Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya WakristoUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
15. (a) Je! kila mmojapo mipigo ya tarumbeta unahusu mwaka mmoja hasa? Eleza. (b) Ni sauti ya nani ambayo imeongezwa kwa ile ya jamii ya Yohana katika kupiga mbiu ya hukumu za Yehova?
15 Kwa kupatana na kuwa kwamba kuna mfululizo wa mipigo ya tarumbeta, maazimio maalumu yalitolewa kwenye mikusanyiko saba kuanzia 1922 mpaka 1928.
-
-
Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya WakristoUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
21. Kunakuwa nini wakati malaika wa pili anapopuliza tarumbeta yake?
21 “Na malaika wa pili akapuliza tarumbeta yake. Na kitu fulani kama mlima mkubwa unaowaka moto kilivurumishwa ndani ya bahari. Na theluthi moja ya bahari ikawa damu; na theluthi moja ya viumbe ambao wamo ndani ya bahari ambao wana nafsi wakafa, na theluthi moja ya mashua zikaharibiwa.” (Ufunuo 8:8, 9, NW) Mandhari hii yenye kuogopesha inatoa picha ya nini?
22, 23. (a) Ni azimio gani lililokuja bila shaka likiwa tokeo la kuvumishwa kwa tarumbeta ya pili? (b) Ni nini kinachowakilishwa na “theluthi moja ya bahari”?
22 Sisi tunaweza kuielewa vizuri juu ya msingi wa ule mkusanyiko wa watu wa Yehova uliofanyiwa Los Angeles, Kalifornia, U.S.A., Agosti 18-26, 1923. Hotuba maalumu alasiri ya Jumamosi iliyotolewa na J. F. Rutherford ilikuwa juu ya kichwa “Kondoo na Mbuzi.” “Kondoo” walitambulishwa waziwazi kuwa wale watu wenye mwelekeo wa uadilifu ambao watarithi milki ya kidunia ya Ufalme wa Mungu. Azimio ambalo lilifuata lilivuta fikira kwenye unafiki wa “viongozi wa kidini waasi-imani na ‘wakuu wa makundi yao,’ ambao ni watu walimwengu wenye mavutano makubwa ya kifedha na kisiasa.” Iliomba ule “umayamaya wa wenye kupenda amani na utaratibu walio katika migawanyiko ya makanisa . . . kujiondoa wenyewe kutoka mifumo hiyo ya kieklesia yenye utovu wa adili ambayo imeitwa na Bwana kuwa ‘Babuloni’” na wajiweke tayari wenyewe “kupokea baraka za ufalme wa Mungu.”
23 Pasipo shaka, azimio hili lilikuja likiwa tokeo la kuvumishwa kwa tarumbeta ya pili.
-