-
Je, Shetani Ni Hadithi Tu au Ni Mtu Halisi Mwovu?Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 15
-
-
Kitabu The Catholic Encyclopedia kinasema: “Kwa miaka elfu moja hivi [fundisho la kwamba Ibilisi alilipwa fidia] lilikuwa sehemu kuu ya mafundisho ya kidini” na fundisho hilo likabaki likiwa imani ya kanisa. Wakuu wengine wa Kanisa, hata na Augustine (karne ya nne na ya tano W.K.), pia walikubali wazo la kwamba ni Shetani aliyelipwa fidia. Hatimaye, kufikia karne ya 12 W.K., wanatheolojia wa Katoliki Anselm na Abelard walikata kauli ya kwamba ni Mungu aliyelipwa dhabihu ya Kristo na wala si Shetani.
Ushirikina Katika Enzi za Kati
Ingawa mabaraza mengi ya Kanisa Katoliki yalibaki kimya sana kuhusu suala hilo la Shetani, mwaka wa 1215 W.K., Baraza Kuu la Nne la Kanisa lilitokeza fundisho ambalo New Catholic Encyclopedia inaliita “tangazo zito la imani.” Kanuni ya Kwanza inasema: “Ibilisi na roho wengine waovu waliumbwa na Mungu wakiwa wazuri, lakini wao wenyewe wakawa waovu.” Kanuni hiyo inaendelea kusema kwamba wao wanajaribu sana kuwadanganya wanadamu. Hili jambo la kuwadanganya wanadamu liliwasumbua watu sana katika Zama za Kati. Ikawa kwamba ni Shetani aliyekuwa akisababisha jambo lolote lile lililoonekana kuwa si la kawaida, kama vile ugonjwa usioeleweka, kifo cha ghafula, au kukosa mavuno. Mwaka wa 1233 W.K., Papa Gregory wa 9 alitoa amri kadhaa dhidi ya wazushi, kutia ndani amri fulani dhidi ya Walusiferi, wale walioonwa kuwa waabudu wa Shetani.
-
-
Je, Shetani Ni Hadithi Tu au Ni Mtu Halisi Mwovu?Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 15
-
-
Lakini katika Baraza la Kwanza la Vatican (1869-1870), Kanisa Katoliki lilikataa jambo hilo na kusisitiza kwamba linaamini kuna Shetani Ibilisi, likirudia kutaja msimamo huo katika Baraza la Pili la Vatican (1962-1965), japo wakati huo si kwa bidii kama katika baraza la kwanza.
Kitabu New Catholic Encyclopedia kinakiri kwamba kirasmi “Kanisa linaamini kuna malaika na roho waovu.” Hata hivyo, Théo, ambayo ni kamusi ya Kifaransa ya Ukatoliki, inakiri kwamba “Wakristo wengi leo hawaoni kama maovu yanasababishwa na ibilisi.” Katika miaka ya karibuni wanatheolojia wa Katoliki wamekuwa katika njia panda, wakitatanika kati ya fundisho rasmi la Katoliki na dhana za watu wengi wakati huu kuhusu Shetani.
-