Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sikukuu
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Kitabu The Worship of the Dead chataja chanzo hiki: “Hadithi za mataifa yote ya kale zinahusiana na matukio ya Gharika . . . Uzito wa hoja hiyo unathibitishwa na maadhimisho ya ile sikukuu ya wafu ya kukumbuka tukio hilo, inayoadhimishwa na mataifa yaliyo karibu, hali kadhalika mataifa yaliyo mbali, yaliyotenganishwa kwa bahari kuu na pia kwa karne nyingi za wakati. Isitoshe, watu wote huadhimisha sikukuu hiyo katika au karibu na siku yenyewe ambayo, kulingana na masimulizi ya Musa, Gharika ilitukia, yaani, siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili—mwezi unaolingana sana na mwezi wetu wa Novemba.” (London, 1904, Kanali J. Garnier, uku. 4) Kwa hiyo, kwa hakika maadhimisho hayo yalianza kwa kuwaheshimu watu ambao Mungu alikuwa amewaharibu kwa sababu ya ubaya wao katika siku za Noa.—Mwa. 6:5-7; 7:11.

  • Sikukuu
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Chapa ya 1910 ya The Encyclopædia Britannica inaeleza hivi: “Siku ya Marehemu Wote . . . siku iliyotengwa katika Kanisa Katoliki ili kuwakumbuka waaminifu waliokufa. Maadhimisho hayo yanategemea fundisho la kwamba nafsi za waaminifu ambazo wakati wa kufa hazikuwa zimesafishwa dhambi zinazoweza kusamehewa, au hazijaondolewa makosa ya zamani, haziwezi kufikia Heri ya Kuona Mungu, na ya kwamba huenda zikasaidiwa kufanya hivyo kwa njia ya sala na kwa njia ya dhabihu ya misa. . . . Imani fulani za watu wengi zinazohusiana na Siku ya Marehemu Wote ni za kipagani na ni za zamani za kale. Wakulima wa nchi nyingi za Kikatoliki huamini kwamba wafu hurudi kwenye nyumba zao za zamani katika usiku wa Siku ya Marehemu Wote na kula chakula cha walio hai.”—Buku la 1, uku. 709.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki