Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ukweli Kuhusu Sherehe Zinazopendwa
    Amkeni!—2001 | Oktoba 8
    • Kichapo The Catholic Encyclopedia chafafanua Siku ya Watakatifu Wote kuwa sherehe ya “kuheshimu watakatifu wote, wanaojulikana na wasiojulikana.” Mwishoni mwa karne ya pili, wale waliodai kuwa Wakristo walianza kuwaheshimu wafia-imani. Waliamini kwamba tayari watu hao walikuwa mbinguni pamoja na Kristo na hivyo waliomba watu hao wasali kwa niaba yao. Mwadhimisho wa kawaida ulianza Mei 13,b 609 au 610 W.K., wakati Papa Boniface wa 4 alipoweka wakfu Pantheon—hekalu la Roma la miungu yote—kwa Mariamu na wafia-imani wote. Markale asema hivi: “Mahali pa miungu ya Roma palichukuliwa na watakatifu wa dini bandia ya Kikristo.”

      Papa Gregory wa 3 (731-741 W.K.), ndiye aliyebadili tarehe hiyo hadi mwezi wa Novemba. Aliweka wakfu kanisa moja huko Roma kwa watakatifu wote kisha akaamuru waheshimiwe Novemba 1. Sababu iliyomfanya abadili tarehe hiyo haijulikani. Lakini huenda ni kwa sababu sikukuu hiyo ilikuwa ikiadhimishwa tarehe hiyohiyo huko Uingereza. Kichapo The Encyclopedia of Religion kinasema kwamba, ‘sherehe ya Samhain iliendelea kupendwa na Waselti kotekote Uingereza wakati Ukristo ulipokuwa ukienea nchini humo. Kanisa la Uingereza lilijaribu kukengeusha fikira za watu kutoka kwa desturi hizo za kipagani kwa kuanzisha sherehe ya Kikristo siku ileile ya sikukuu ya Samhain. . . . Huenda sherehe ya Siku ya Watakatifu Wote iliyoanza katika enzi za kati nchini Uingereza ilienea upesi katika makanisa ya Kikristo ulimwenguni pote.’

      Markale anataja kwamba uvutano wa watawa wa Ireland ulikuwa ukiongezeka wakati huo kotekote katika Ulaya. Pia, kichapo New Catholic Encyclopedia chasema hivi: ‘Wakazi wa Ireland walisherehekea sikukuu muhimu tarehe moja ya mwezi. Kwa kuwa majira ya baridi kali ya Waselti yalianza Novemba 1, basi yamkini siku hiyo ingefaa kuwa sikukuu ya watakatifu wote.’ Hatimaye, Papa Gregory wa 4 aliifanya siku hiyo kuwa sikukuu ya kimataifa mnamo mwaka wa 835 W.K.

  • Ukweli Kuhusu Sherehe Zinazopendwa
    Amkeni!—2001 | Oktoba 8
    • Kanisa lilikubali imani za kipagani kana kwamba ni za Kikristo kwa sababu lilishindwa kuwazuia waumini kufuata imani hizo. Kichapo The Encyclopedia of Religion chakazia jambo hilo kwa kusema hivi: ‘Sherehe ya Kikristo ya Siku ya Watakatifu Wote, ni ya kukumbuka watakatifu wanaojulikana na wasiojulikana wa dini ya Kikristo kama vile sherehe ya Samhain ilivyoheshimu na kusifu miungu ya Waselti.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki