-
Mahali pa Kubatizia Ushuhuda wa Desturi IliyosahaulikaAmkeni!—2007 | Septemba
-
-
“ABATIZWA kwa Kuzamishwa Kwenye Kanisa Kuu,” ndivyo kilivyosema kichwa cha gazeti moja la Ufaransa mnamo 2001. Hata hivyo, picha katika makala hiyo ilionyesha muumini mpya Mkatoliki akisimama ndani ya kidimbwi kikubwa cha ubatizo, maji yakiwa yamemfikia magotini na askofu Mkatoliki akimmwagilia maji kichwani. Tukio hilo ambalo hurudiwa sehemu nyingi ulimwenguni linaonyesha utamaduni wa Kanisa Katoliki tangu Baraza la Pili la Vatican lianze kubatiza waumini wapya kwa kutozamisha mwili wote.
-
-
Mahali pa Kubatizia Ushuhuda wa Desturi IliyosahaulikaAmkeni!—2007 | Septemba
-
-
Kuzamisha Kabisa au Nusu?
Je, watu walizamishwa kabisa katika majengo hayo ya zamani ya kubatizia? Wanahistoria fulani Wakatoliki wanakataa jambo hilo, wakidai kwamba kubatiza kwa kunyunyiza (kummwagilia mtu maji kichwani) kulifanywa mapema katika historia ya Kanisa Katoliki. Pia wanasema kwamba vidimbwi vingi havikuzidi kina cha mita 1 na hivyo havikuwa na kina cha kutosha kumzamisha kabisa mtu mzima. Ensaiklopedia ya Kikatoliki inasema kwamba huko Poitiers “anayebatiza [kasisi] angesimama kwenye ngazi ya tatu bila kugusa maji.”
Hata hivyo, michoro ya ubatizo huo huonyesha kwamba ilikuwa kawaida kuzamishwa kikamili. Michoro hiyo ilionyesha maji yakiwa yamemfikia mtu anayebatizwa kifuani au shingoni kabla ya ubatizo. (Ona picha juu.) Je, ingewezekana kumzamisha mtu kikamili ikiwa kina cha maji kilimfikia kiunoni mtu mwenye kimo cha kawaida? Kitabu kimoja kinadokeza kwamba kidimbwi kingezibwa hadi mtu anayebatizwa aliyepiga magoti au kuchuchumaa azamishwe.a Pierre Jounel profesa wa desturi na sherehe za Kikatoliki huko Paris, anasema: Mtu anayebatizwa “alisimama maji yakiwa yamemfikia kiunoni. Akiweka mkono juu ya kichwa chake, kasisi au shemasi alimwinamisha majini ili mwili wote uzamishwe.”
Vidimbwi vya Ubatizo Vyapunguzwa Ukubwa
Hatimaye ubatizo wa kawaida uliokuwa umefanywa katika nyakati za mitume ulibadilika na kuanza kuhusisha desturi yenye kutatanisha, nguo na ishara za pekee, sala za kufukuza pepo, kubariki maji, kukariri kanuni ya imani, na kutiwa mafuta. Desturi ya watu kuzamishwa nusu ikaendelea kuenea. Vidimbwi vya ubatizo vilipunguzwa vikawa nusu ya ukubwa wa awali. Kwa mfano, huko Cazères, kusini mwa Ufaransa, kidimbwi cha awali kilichokuwa na kina cha mita 1.13 kilipunguzwa hadi kikawa na kina cha nusu mita hivi kufikia karne ya sita. Baadaye, karibu karne ya 12, Wakatoliki waliacha kuwazamisha watu nusu na wakaanza kuwanyunyizia maji. Kulingana na msomi Mfaransa Pierre Chaunu, hilo lilitokea kwa sababu “kuwabatiza watoto kulikuwa kumeanza kuenea katika nchi zenye hali mbaya ya hewa, kwa kuwa haingewezekana kumtumbukiza mtoto mchanga ndani ya maji baridi.”
Mambo hayo yalisababisha vidimbwi kuwa vidogo hata zaidi. Katika uchunguzi wake kuhusu historia ya ubatizo, mwanahistoria Frédéric Buhler anasema: “Uchimbuzi wa vitu vya kale, hati, na sanaa, kwa ujumla zinaonyesha kwamba njia za kuwabatiza watu zilibadilika hatua kwa hatua kutoka kuwazamisha kabisa watu wazima katika karne za kwanza za Ukristo, kuwazamisha nusu, kuwazamisha watoto kabisa, na hatimaye kuwanyunyizia watoto wachanga maji.”
Leo, zoea la kuwazamisha nusu watu wazima linazidi kuwa maarufu, kwa kuwa vidimbwi vikubwa zaidi vya kubatizia vinajengwa.
-