Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Pigano la Biblia ya Kifaransa la Kuokoka
    Amkeni!—1997 | Desemba 8
    • Baadaye, kanisa lililaumu Waldo na wafuasi wake likiwaita wazushi, na watawa wa kiume wakachoma tafsiri alizokuwa ameagiza. Kuanzia hapo na kuendelea, kanisa lilikinza kila jitihada ya kufanya Neno la Mungu lipatikane mikononi mwa watu wa kawaida.

      Kanisa lilidhihirisha hila yake mwaka wa 1211 kwa kuchoma Biblia katika jiji la Metz, mashariki ya Ufaransa. Mwaka wa 1229 Baraza la Toulouse lilikataza kabisa watu wa kawaida kutumia Biblia za lugha za wenyeji katika lugha yoyote ile. Hilo lilifuatwa mwaka wa 1234 na Baraza la Tarragona, Hispania, ambalo lilikataza mtu kuwa na Biblia katika yoyote ya lugha za Kiroma (lugha zilizotokana na Kilatini), hata na makasisi.

  • Pigano la Biblia ya Kifaransa la Kuokoka
    Amkeni!—1997 | Desemba 8
    • Kanisa Katoliki lilikinza badiliko lolote katika mbinu zake, lakini lilikuwa linashindwa. Katika karne yote ya 19, mapapa walitoa mfululizo wa maagizo yakipinga kikatili Biblia za lugha ya wenyeji. Kufikia mwisho-mwisho wa 1897, Papa Leo wa 13 alisisitiza tena kwamba “tafsiri zote za Vitabu Vitakatifu zilizofanyizwa na mwandikaji yeyote yule asiye Mkatoliki na kwa lugha yoyote ya kawaida zimekatazwa, hasa zile zilizochapishwa na sosaiti za Biblia, ambazo zimelaumiwa na Papa wa Roma mara kadhaa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki