Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jinsi Biblia Ilivyotufikia—Sehemu ya Pili
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 15
    • Miali ya moto ilipaa juu fueli zaidi na zaidi iliporundikwa kwenye moto mkubwa sana. Lakini huo haukuwa moto wa kawaida. Huo moto mkubwa ulikuwa ukiongezwa Biblia huku makasisi na maaskofu wakitazama. Lakini kwa kununua Biblia ili kuziharibu, askofu wa London bila kujua alimsaidia mtafsiri, William Tyndale, kugharimia chapa zaidi!

  • Jinsi Biblia Ilivyotufikia—Sehemu ya Pili
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 15
    • Katika barua aliyomwandikia Papa John wa 23 mwaka wa 1412, Askofu Mkuu Arundel alirejezea “yule jamaa mwenye kustahili kudharauliwa na msumbufu, John Wycliffe, akumbukwaye kuwa mtu mwenye kuchukiza sana, mwana wa yule nyoka wa kale, aliyefananisha kimbele na aliye mwana wa mpinga-Kristo.” Akifikia upeo wa shutumu lake la hadharani, Arundel aliandika hivi: “Ili kujaza kabisa kipimo cha uovu wake, alibuni tafsiri mpya ya maandiko katika lugha ya kienyeji ya kufaa lengo fulani.” Kwa kweli, lililowakasirisha zaidi viongozi wa kanisa lilikuwa kwamba Wycliffe alitaka kuwapa watu Biblia katika lugha yao wenyewe.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki