-
Kitabu Kinachopinga Vitabu VingineAmkeni!—2003 | Septemba 8
-
-
Nyongeza ya kitabu hicho iliorodhesha tafsiri za Biblia zilizopigwa marufuku, na ilitaja waziwazi kwamba tafsiri zote za lugha za kienyeji zilikuwa zimepigwa marufuku.
Ingawa tayari vitabu fulani vilikuwa vimepigwa marufuku, “kupitia maagizo hayo yaliyowaathiri Wakatoliki wote, kanisa lilitoa tangazo rasmi la kwanza lililopinga kuchapisha, kusoma, na kuwa na Biblia Takatifu katika lugha ya kienyeji,” asema Gigliola Fragnito, mwalimu wa historia ya kisasa kwenye Chuo Kikuu cha Parma, Italia.
-
-
Kitabu Kinachopinga Vitabu VingineAmkeni!—2003 | Septemba 8
-
-
Orodha hiyo iliyokuwa imetayarishwa na baraza la Index na kutolewa rasmi na Clement wa Nane mnamo Machi 1596, ilizuiliwa kufuatia ombi la Ofisi Takatifu hadi wakati ambapo ingekuwa na nguvu zaidi za kupiga marufuku usomaji wote wa Biblia katika lugha za watu wa kawaida.
-
-
Kitabu Kinachopinga Vitabu VingineAmkeni!—2003 | Septemba 8
-
-
Biblia Katika Lugha za Kawaida
Historia ya kitabu Index yaonyesha kwamba kati ya “vitabu vyote vyenye kudhuru,” kimoja hasa ndicho kilichowatia hofu makasisi—Biblia katika lugha za kawaida. Katika karne ya 16, “tafsiri zipatazo 210 za Biblia nzima au Agano Jipya” ziliorodheshwa katika vitabu Index, aeleza mtaalamu Jesús Martinez de Bujanda. Katika karne ya 16, Waitaliano walijulikana kuwa wasomaji wenye bidii wa Biblia. Hata hivyo, kitabu Index, pamoja na sheria zake kali zilizopiga marufuku Maandiko katika lugha za kienyeji, ziliathiri sana maoni ya taifa hili kuelekea Neno la Mungu. “Yakiwa yamepigwa marufuku na kufutiliwa mbali eti kwa kuwa yanasababisha uasi, hatimaye Waitaliano waliyaona Maandiko matakatifu kimakosa kuwa maandishi ya waasi wa kidini,” asema Fragnito, kisha aongezea: “Wakatoliki wa kusini mwa Ulaya wangeweza tu kupata wokovu kupitia ukatekisimu,” na “watu wasiokomaa ndio waliotakikana zaidi kuliko watu waliokomaa kidini.”
Ni katika mwaka 1757 tu ndipo Papa Benedict wa 14 alipoidhinisha usomaji wa ‘tafsiri za Biblia za lugha za kienyeji ambazo ziliidhinishwa na Dayosisi ya Papa.’
-